FOCAC yaweka mfano mzuri kwa ushirikiano wa kimataifa na Afrika

FOCAC yaweka mfano mzuri kwa ushirikiano wa kimataifa na Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
f636afc379310a551b0eaed3ba4543a9822610ea.jpg

Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) umefanyika hivi karibuni mjini Dakar, Senegal. Tangu kuanzishwa kwa jukwaa hilo, ushirikiano kati ya China na Afrika umepata mafanikio makubwa, na kuwa mfano mzuri kwa ushirikiano wa kimataifa na Afrika.

Ili kuimarisha zaidi ushirikiano wa kirafiki, kukabiliana na changamoto, na kutafuta maendeleo kwa pamoja, China na Afrika zilianzisha FOCAC Oktoba mwaka 2000. Baada ya zaidi ya miaka 20, jukwaa hilo limepata mafanikio makubwa katika kuendeleza ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Kwa upande wa biashara, China imeendelea kuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 12 mfululizo. Tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imeongezeka kuwa dola bilioni 200 za Kimarekani mwaka 2020 kutoka dola bilioni 10 za mwaka 2000, na kuongezeka kwa mara 20.

Katika mkutano huo uliofanyika nchini Senegal, Rais Xi Jinping wa China ametangaza kuwa, China itajitahidi kuagiza bidhaa za Afrika kwa dola bilioni 300 za Kimarekani katika miaka mitatu ijayo. Hii ni ahadi ya dhati ya China kuhimiza maendeleo ya biashara, na kuboresha muundo wa biashara kati ya pande hizo mbili.

Kwa upande wa miundombinu, Afrika imekuwa soko la pili la China kwa miradi ya ujenzi wa miundombinu katika nchi za nje. China imetekeleza miradi mingi ya miundombinu kufuatia mahitaji ya nchi za Afrika. Takwimu zinaonyesha kuwa tangu kuanzishwa kwa FOCAC, makampuni ya China yameongeza na kuboresha zaidi ya kilomita 10,000 za reli na karibu kilomita 100,000 za barabara barani Afrika, na kutoa nafasi za ajira zaidi ya milioni 4.5. Kwa upande wa uwekezaji, uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika umezidi dola bilioni 43.4, za kimarekani, na kushika nafasi ya nne kwa ukubwa wa uwekezaji barani Afrika. Katika mkutano wa Dakar, China imeahidi kuongeza uwekezaji barani Afrika angalau kwa dola bilioni 10 za Kimarekani katika miaka mitatu ijayo.

Katika mapambano dhidi ya janga la COVID-19, China na Afrika zimeonesha kikamilifu roho ya jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Mnamo Juni 2020, Rais Xi aliandaa mkutano maalum wa kilele wa China na Afrika dhidi ya janga hili kwa njia ya video. Hadi sasa China imetoa shehena 120 za msaada wa vifaa vya kukabiliana na janga hilo kwa nchi 53 za Afrika, na kutuma timu za wataalam wa matibabu katika nchi 17 za Afrika. Katika mkutano wa Dakar, Rais Xi ametangaza kwamba China itatoa dozi nyingine bilioni 1 za chanjo kwa Afrika, na pia itazisaidia nchi za Afrika katika kutekeleza miradi 10 ya afya, na kupeleka wataalam 1,500 wa matibabu kwa nchi za bara hilo.

China pia imefanya ushirikiano wa kina na Afrika katika nyanja nyingine nyingi zikiwemo kupunguza umaskini, maendeleo ya viwanda, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kudumisha amani na usalama, na kuendeleza uchumi mpya wa kidijitali, na kupata mafanikio mazuri.

Lengo kuu la ushirikiano kati ya China na Afrika siku zote ni maslahi ya kimsingi ya watu wa pande hizo mbili. Licha ya kuleta manufaa halisi kwa watu wa China na Afrika, ushirikiano huo pia umeweka mfano mzuri kwa ushirikiano wa kimataifa na Afrika.
 
Wavimba Macho ndiyo wanaikomboa Africa
 
Back
Top Bottom