KERO Foleni ya kuweka gesi Dar kwenye magari ni tatizo

KERO Foleni ya kuweka gesi Dar kwenye magari ni tatizo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Mchangamoto tunaopitia wakati wa kujaza gesi kwenye magari ni kero kubwa ya foleni inayotokana na wingi wa wenye uhitaji huku sehemu za kujazia zikiwa chache.

Hicho ni kikwazo kikubwa pia kwa madereva hasa wale ndugu zangu wa Taksi Mtandao kwa kuwa wanatumia muda mwingi kwenye foleni ya gesi kiasi kwamba inakuwa kama mateso na sio furaha kwao, wanapoteza wateja wakisubiri gesi.

Najua siku zinavyozidi kwenda foleni itakuwa kubwa mara tano ya ilivyo sasa kwa kuwa nishati ya mafuta mambo yanazidi kuwa magumu kutokana na bei kupanda kila kukicha.

Pia, soma;

Serikali yasema inajenga vituo vingine vitatu vya Nishati ya gesi ya magari
 
yote hii ni kwa kuwa tunaweka VIONGOZI kama MUME WA SPIKA kwenye EWURA ambao wananyima vibali watu kufunga sheli za gesi wakati hata wenye masheli pia waliomba kuweka! swali ni Je mnazuia vibali kwa faida ya nani! au roho mbaya tu! kumtumbua mnaogopa kwa kuwa ni mume wa spika! Mungu atatenda tu ipo siku
 
Kwani hivyo vituo viko wapi? Na ni vingapi kwa hapa dar? Na je inje ya dar vipo?
 
Gari moja inachukua muda gani kujazwa huu mtungi? Naulizia hivi vigari vidogo maaan unavikuta telee kwenye foleni ya kuweka hiyo gesi hadi unaona haya ni mateso ndugu zetu waliofunga mfumo wa gesi wanapitia
 
Back
Top Bottom