Bado Hujasema
Member
- Dec 1, 2024
- 12
- 14
Sisi Wakazi wa Mikumi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro tuna kero ya muda mrefu ya foleni ya magari makubwa ya mizigo katika Mizani ya Mikumi, hali ambayo inatufanya kuhofia kutokea kwa ajali katika eneo hilo.
Foleni hiyo inatokana utaratibu wa askari wakati wa ukaguzi wa magari hayo mpaka tunahofia kuwepo kwa viashiria vya rushwa, kwanini eneo hilo magari yakae muda mrefu maana inaleta kero kwa watumiaji wengine wa barabara kama magari madogo, bajaji, pikipiki mpaka kwa watembea kwa miguu.
Kibaya zaidi kuna sehemu ya kupaki hayo malori ambayo ni jirani kabisa na mizani hiyo, kwanini magari yasiwe yanatoka kwa utaratibu na mpangilio ili foleni isiwepo au kuna kitu nyuma ya pazia ambacho sisi hatukijui.
Unakuta mtu mwenye gari dogo anakaa saa kadhaa au alazimishe kupita, la sivyo mtu kama si mzoefu au mgeni wa eneo hilo hawezi kupita pale.
Tunaomba mamlaka husika zitupie jicho eneo hilo ili foleni ma mkusanyiko wa magari upungue kama si kuisha kabisa iwe pawe salama kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Siku kutakuja kutokea ajali kubwa sana halafu Serikali ije itupiwe lawama wakati uwezekano wa watu kufanyakazi yao wapo au watu kulifanyia kazi wanaweza askari wanaokagua eneo hilo wafanye kazi yao kuondoa foleni na mkusanyika wa magari katika eneo hilo.