A
Anonymous
Guest
Wastani wa Malori zaidi ya 1,000 hutoka kila siku Dar es Salaam kuelekea mikoa mbalimbali ya Tanzania na Nchi Jirani. Upanuzi wa barabara hiyo kutoka Ubungo hadi Kimara ni suluhisho la muda mfupi tu. Foleni itahamia Kibaha Mjini.
Suluhisho la muda mrefu
Naishauri Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025 itenge bajeti ya kujenga escape route ya malori itakayopita kutoka Dar es Salaam, Kibaha, Kisarawe hadi Chalinze, na zitengenezwe parking za malori za kutosha za kulipia katika njia hiyo ili kunusuru msongamamo wa Malori ndani ya Jiji la Dar.
Malori yawe yanaingia mjini pale yanapokuja kupakia tu na si vinginevyo, hili likifanikiwa naamini tatizo la foleni Dar es Salaam litapungua kwa zaidi ya Asilimia 60.
Suluhisho la muda mfupi
Malori yazuiwe kutoka mpaka Saa Sita Usiku, yasitoke muda wa peak ambapo yanakutana na magari mengine ya umma na binafsi yanayotoka kazini na kusababisha msongamano wa magari. Kama ambavyo Alfajiri Malori huzuiwa, yanaweza kuzuiwa na jioni pia.
Mfano wa hali inavyokuwa siku nyingine