SI KWELI Folic Acid si salama kwa Wajawazito, wanashauriwa waache kuitumia

SI KWELI Folic Acid si salama kwa Wajawazito, wanashauriwa waache kuitumia

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1

​
1769752077517.png


Nimekutana na hii video ya mtu mmoja ambaye ni Fitness trainer, anashauri wanawake wajawazito wasitumie Folic Acid maana itawaletea matatizo kwa baadae.

Nimeogopa sana aisee. Ujumbe huu ni sahihi kweli?
 
Tunachokijua
Ujumbe unaotolewa kwenye Video hii, ambao pamoja na Mambo mengine unatoa ushauri kwa Wanawake Wajawazito kuepuka Matumizi ya Virutubisho vya 'Folic Acid' ili kujilinda dhidi ya Magonjwa Mbalimbali Si ya Kweli

Kwa mujibu wa Miongozo ya Shirika la Afya Duniani (WHO), Kituo cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa (CDC), Wizara ya Afya Tanzania pamoja na Tafiti Mbalimbali zinazohusu Afya ya Uzazi, Matumizi ya Folic Acid huzuia kutokea kwa kasoro za kuzaliwa kwenye Ubongo na Uti wa Mgongo wa mtoto.

Shirika la Afya Dunia (WHO) linaeleza kuwa zaidi ya asilimia 40 ya wanawake wajawazito duniani wana upungufu wa damu (anaemia). Angalau nusu ya tatizo hili la upungufu wa damu linaaminika kusababishwa na upungufu wa madini ya chuma (iron).

Na hivyo wanapendekeza kuwa Wanawake wajawazito wanahitaji madini ya chuma na asidi ya foliki (Folic Acid) kwa kiasi cha ziada ili kukidhi mahitaji yao ya lishe pamoja na mahitaji ya mtoto anayekua tumboni.

Upungufu wa madini ya chuma na asidi ya foliki wakati wa ujauzito unaweza kuathiri vibaya afya ya mama, ujauzito wenyewe, pamoja na ukuaji wa mtoto.

Aidha, humsaidia Mama kuongeza damu, husaidia ukuaji mzuri wa kondo la Uzazi (Placenta) na hupunguza hatari ya matatizo kama kuharibika kwa Mimba, mtoto kuzaliwa Njiti au mwenye uzito mdogo.
Leta ujinga wenu huo

Mtazaa watoto mdomo wazi,mgongo wazi ,wenyezika ,vichwa vikubwa mpaka mkome
 
Back
Top Bottom