Fomu ya Polisi No. 3 (PF3)

MZIMU

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
4,058
Reaction score
1,373
Mtu anagongwa na Gari, anawahishwa Hospital, Madaktari wana kataa kumpokea mpaka apewe form ya Pf3 kutoka police. Mgonjwa anarudishwa Police kupewa form ya PF3. Baada ya kupata form ya PF3, anarudishwa Hospital. Mgonjwa anapofika hospitali kwa Mara ya Pili, amekata roho.

Je hii form inafaida kwa mgonjwa??
 
Nahisi hii kitu ifanyiwe Mabdiliko kisheria,Kiukweli mm mwenyew huwa nachanganyikiwa mtu anapokuwa,anagugumia kwa Maumivu ya kisu,kuvunjika na mapanga n:k.chakushangaza hata kama anaishi karibu na Hosp itabidi apelekwe kituo cha polisi Km 4-8,then anarudishwa tena.
 
kabisa sheria inabidi ifanyiwe marekebisho ukute mtu ameumia badala ya kuwahishwa kwenye huduma akatibiwe anapelekwa kituo cha polisi,kama kuna ulazima zaidi wa mtu aliyeumia kuanzia vituo vya polisi basi serikali ijenge vituo vya polisi kila kulipo na hospitali ili kuepusha usumbufu zaidi kwa wagonjwa na kupewa huduma haraka zaidi
 
halafu mie mpk leo cjajua ni nini hasa uhusiano kati ya mjeruhiwa,daktari na iko ki PF3...mi naona usumbufu tu coz inawezekana kabisa mtu kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na daktar na kisha kupatiwa huduma ya kwanza,hlf ndipo taratibu nyengine km iyo pf3 ndo zifuate.
 
Aim ya pf3 ni dokumenti inayoweza kutumika ka ushahidi baadae Mahakamani kwamba X alijeruhiwa vibaya na Y. hivyo kwa kupitia dokumenti hiyo ndipo kesi inaweza kufunguliwa..
kwa hiyo wazo la pf3 ni zuri katika kusaidia kufikisha mashitaka ya kujeruhi mahakamani.

siku zote challenge hujitokeza. challenge iliyopo ni pale mtu anpokuwa amepata shida afu yupo mahututi na anatakiwa kupatiwa huduma.. na kituo cha polisi kipo mbali na hospital.. na madaktari wanalazimika kufata sheria ya kumuhudumia mtu huyo mara tu baada ya kuona pf3.

hivyo ni kuomba vyombo vya sheria vijaribu ku ammend police rules zinazotoa ulazima wa izo form (pf3) kuwa ziwe zinapatikana katika mahospitali.. ili kurahisisha mambo. na kuwa na afisa wa polisi katika kila hospital ili kutekeleza ilo swala.
asanteni.
 

Nadhani ingesaidia sana kuaoka roho za majeruhi wengi wanaoachwa bila huduma ya kwanza na kufariki kabla ya matibabu .
Kama lengo ni uchunguzi na uhakiki wa kutendeka kwa jinai-Dr anayempokea na kumhudumia majeruhi sheria imtambue kuwa anamamlaka ya kujaza hiyo PF3 na sharti aiarifu Kituo cha Polisi kwa simu au Kitungo cha dharura cha Polisi kwa simu kuwa amepokea Majeruhi na ametoa huduma ya kwanza/matibabu ili polisi wachukua hatua stahiki kuanzia hapo.

Siku hizi mawasiliano siyo shida hata kidogo !
 
Upo sawa kabisa.. Japo swala la simu lilishashindikana. kikubwa ni kuzifanya izo form ziwe zinapatikana mahospitalini.. waweke kitengo kidogo cha afisa polisi wa kuzisimamia ili kupunguza adha ya kwenda kituo cha polisi.
 
hivyo ni kuomba vyombo vya sheria vijaribu ku ammend police rules zinazotoa ulazima wa izo form (pf3) kuwa ziwe zinapatikana katika mahospitali.. ili kurahisisha mambo. na kuwa na afisa wa polisi katika kila hospital ili kutekeleza ilo swala.
You hit the nail on the head! Indeed the intention of instituting the PF3 form might have been very good in the sense that it forms the basis of following-up a crime. However, in the long-run the means is being misused. The forms should be made available at the hospitals so that priority goes to attending to the patient; and afterwards the doctor completes the form; and later on the police do their duty. the sequence should be in that order.
 
Kitengo cha PF3 kiwekwe kwenye mahospitali.. mapolisi wawe na kitengo hospitalini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…