Nimesikia kupitia redio moja ya Mkoani Iringa (bila kukosea ni Ebony FM) ya kwamba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetoa fomu za kurudia Mtihani wa Kidato cha Nne - 2012 kwa wanafunzi waliopata Daraja Sifuri, fomu hizo zinauzwa kwa gharama ya Tsh. 10,000. Kuna vituo maalumu vimeteuliwa kwa ajili ya mauzo. Kwa Mkoani Iringa, fomu hizo zinapatikana hapo Ebony FM.
Kwa mikoa mingine sijui nini kinaendelea, ila mnaweza kuijuza jamii ya Kitanzania. Hii ni fursa nyingine tena kwa wale walioangukia pua ya kujinasua.