Food poisoning sumu kwenye chakula

Food poisoning sumu kwenye chakula

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Ni jambo la kawaida sana kwa baadhi ya Watu kuumwa tumbo na kuhara baada ya kula chakula Fulani,---- watu hawali mbogamatunda,nyama au samaki wa aina Fulani kwasababu wakila Tumbo linauma,na wengine hata

kutapika.Wataalam wa afya wanasema hii husababishwa na hali ya mwili wa mtu kutokukubaliana na kitu Fulani kilicho katika chakula kile.inaweza kua ni kemikali ya asili iliyo katika chakula au ,aina fulani ya vijidudu (vyenyemanufaa) Na

wakati mwingine husababishwa na vijidudud viharibifu vilivyomo katika chakula.

Nitoe mfano :Mimi situmii kabisa mafuta ya pamba,nikila chakula kilichopikwa na mafuta ya pamba,naumwa sana tumbo na kuhara adi pale kile chakula kitakapoisha kabisa tumbono,mara nyingi inanichukua siku mbili adi Tatu Tumbo langu kurudi katika hali ya kawaida..

Wengi mtakubaliana na mimi nikisema mara nyingi sana watu huumwa tumbo baada ya kula vyakula kwenye sherehe,au hotelini.Na wengi hukwepa kula kachumbari,salads na matunda wanapokula nje ya nyumbani.Sababu inayofanya wakwepe kula salads na kachumbari ni kwasababu hawaamini usafi wa mboga,matunda pamoja na mikono ya Yule aliyeandaa,na kwasababu vyakula hivyo huliwa vibichi watu hawaamini usalama wake.Hali ya kuumwa tumbo inayosababishwa na chakula huitwa Food poisoning yaani Sumu ndani ya chakula



Maana ya food poisoning

Food poisoning ni ugonjwa unaosababishwa na ulaji na unywaji wa chakula chenye viumbe waharibifu kama vile bacteria,virusi,au vimelea vya maradhi na wakati mwingine husababishwa na kemikali zinazopatikana ndani ya chakula fulani,au katika samaki na mimea yenye sumu ya asili.


Mara Nyingi viumbe viharibifu hupatikana kwenye vyakula vibichi kama nyama ,kuku,samaki,na mayai na kwenye mboga za majani na matunda yasiooshwa vizuri. lakini vinaweza kusambaa kwenye aina yoyote ya chakula.pia vinaweza

kukua kutoka kwenye chakula chenyewe hasa pale chakula kinapotunzwa vibaya.Lakini pia food poisoning huweza tokea pale mtu anashika chakula bila kuosha mikono,kwani kunauwezekano wa kubeba vijidudu waaribifu kutoka kwenye vyanzo vingine.Baadhi ya Vijidudu vinavyosababisha food poisoning ni Salmonella na E coli.


Mara nyingi food poisoning si ugonjwa unaokuja kwanguvu,Kawaida huisha wenyewe baada ya siku chache,baada ya mwili kuondokana na vijidudud vilivyosababisha ugonjwa au kuumwa huko.Lakini kuna aina ya food poisoning ambazo ni mbaya sana na zinaweza ata kuchukua maisha ya mtu,hivyo ni vyema kuwai hosipitali kwa ajili ya tiba.


Dalili za food poisoning


Dalili kuu ya food poisoning ni kuhara.lakini pia unaweza kutapika, kua na maumivu ya tumbo(kitaalamu hujulikana kama

stomach flu). Aidha dalili hizo mara nyingi huambatana na maumivu ya misuli, homa, kutetemeka mwili na kuhisi kuchoka. Dalili hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu kutokana na aina ya vijidudud wanaosababisha ugonjwa pamoja ya uwezo wa kinga zake za mwili kukabiliana na ugonjwa.


Hatua ya kuhara na kutapika, husaidia mwili kuondoa sumu au vijidudu vya maradhi katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula (digestive tract) na hivyo kuzizuia sumu au vijidudu vya maradhi kuingia katika mfumo wa damu.Kuhara na

kutapika kwingi husababisha mwili kuishiwa maji hivyo ni vyema kunywa maji mengi.Kukauka mdomo na koo,kuumwa kichwa,na mkojo mchafu ni dalili za kuishiwa maji mwilini.Watoto wadogo na wazee huishiwa maji mwilini kwa haraka sana,ni vyema kuwatizama kwa karibu wanapopata food poisoning.Mama mjamzito anapohisi kua amepata food poisoning ni vyema kwenda hosipitali haraka.
Katika picha.Bibi anaongezewa maji baada ya kuhara na kutapika kwa muda mrefu kulikosababishwa na uyoga wenye sumu.


Baahi ya namna ambazo vijidudu huingia kwenye chakula


  • Nikawaida kabisa kukuta vijidudu vya maradhi katika utumbo wa wanyama ambao binadamu hutumia nyama yao, kama ,ng’ombe,kuku,samaki,mbuzi na nguruwe kutoka na ualisia wa vyakula wanavyokula.Hivyo ni vyema kujua kwamba nyama ya utumbo huwa na vijidudu vingi vinavyoweza kuleta food poisoning.Wakati mwingine vijidudu hivyo husambaa kwenye sehem nyingine au vipande vingine vya nyama wakati wa uandaaji wa nyama machinjioni.
  • Kama mboga na matunda zinamwagiliwa na maji machafu hasa yale yenye uchafu wa chooni au wa zizi basi vijidu hutoka kwenye maji hayo machafu na huingia katika mboga na matunda,Pia endapo mboga na matunda vitaoshwa na maji machafu Vijidudu vitabaki kwenye mboga na matunda hayo.
  • Pale mtu anaposhika chakula kwa mikono michafu yenye vijidudu,vijidudu hubaki kwenye chakula.
  • Inzi anapotua kwenye kwenye chakula au uchafu wenye vijidudu huvibeba.na pale atakapotua kwenye chakula kisafi huacha vijidudu hivyo.
  • Wakati mwingine vijidudu hutoka hewani na kuingi kwenye chakula.kuna navaijidudu vingi sana hewani na baadhi huweza sababisha food poisoning pale wanapoingia kwenye chakula
Wakati mwingine ni ngumu kugundua umepata food poisoning,kwani mra nyingi ugonjwa huu hauji kwanguvu.Mara nyingi tumbo huuma na kisha kuhara,mara nyingi utasikia watu wakisema chakula kimewachafua tumbo.Endapo unahisi au umepata dalili hizi ni vyema kuwauliza wale mliokula nao chakula hicho kama nao wanapata dalili hizo,hii itasaidia kujua kama umepata food poisoning ili uweze kuchukua hatua mapema.
Dalili za food poisoning huanza kujitokeza kati ya saa moja hadi matatu baada ya kula chakula kisichofaa, Na wakati mwingine mtu hawezi kujisikia vibaya hadi siku chache baadaye

Namna ya kuepuka food poisoning


Unaweza chukua hatua zifuatazo ili kuepukana au kupunguza uwezekano wakupata na food poisoning.


  • Osha mikono baada ya kutumia chooo,na kabla ya kushika chakula chochote.
  • Osha mboga na natunda vizuri
  • Epuka mboga za majani zilizolimwa karibu na sehem za taka au zinazomwagiwa maji machafu
  • Pika nyama vizuri na uakikishe imeiva vizuri
  • Unapoandaa utumbo ,hakikisha umeuosha vizuri,na upike kwa muda mrefu ili kuuwa vijidudu wote
  • Epuka kula chakula kilichokaa wazi kwa muda mrefu
  • Pasha moto vizuri kabla ya kula kipioro
  • Jokofu lako liwe na ubaridi wa nyuzi joto 40 na freezer iwe na 0
  • Epuka kutunza kiporo frijini zaidi ya siku nne,endapo unataka kikae zaidi ya apo basi kiweke kwenye freezer.

    Mboga zilizopandwa katika mazingira safi

Watoto ni kundi ambalo liko katika hatari kubwa sana ya kupata food poisoning,ni jukumu la kila mzazi na kila mtu mwenye uelewa juu ya foodpoisoning kuchukua hatua ili kusaidia kuwaepusha watoto na tatizo hili kwa kuwafundisha na kuwapa ufaham juu ya tatizo hili na pia kuwatizama kwa karibu.

Zingatia usafi,uilinde familia yako .UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU FOOD POISONING(SUMU KWENYE CHAKULA) | TOLLYzKITCHEN
 
Back
Top Bottom