Sie tunaoandika ni kama tunajipendelea vile kwani wengi wetu kama sio wote tunaamini uzuri ama ubovu wa movie unategemea sana na script. Tunaamini kwamba, script ikishakuwa mbaya, na bahati mbaya ukapata Director mbaya, au hata kama ni mzuri akaacha kuibomoa script, basi hata kama utachukua waigizaji kutoka Hollywood, movie itakuwa mbaya tu; piga ua! Lakini ukishakuwa na tight script, hata kama utachukua amateur actors, filamu/movie nayo itakuwa tight. WHY? Suala la kuandika ni inner feelings inayotegemeana sana na talent especially kwa sehemu ambayo haina formal screenwriting training. Kama script inasema Character X anakimbia kutokana na hofu lakini badala yake akawa anakimbia kama vile anafanya mazoezi, ni rahisi Director kuona na kumwambia No that way, kimbia huku mara moja moja ukiwa unaingilia nyuma kuonesha una hofu! lakini si rahisi mtu kumwambia no andika hivi! coz anafanya hivyo huku akiwa amejifungia chumbani kwake na alichokiweka kwenye karatasi ndiyo his/her inner feeling! So, mwandishi anapoandika wakati hamna well structured plots zilizobeba important plot factors such as well framed events zenye bums za hapa na pale, no clear reason why particular even happens, no dramatic conflict, etc! Katika mazingira kama hayo always utatengeneza movie ambayo iko very flat and boring coz the script itself is flat and boring. Hata kama utachukua waigizaji kutoka Hollywood, kama nilivyosema movie itakuwa mbaya tu ima faima!
Tatizo hapa kwetu, mtu akicheza filamu mbili tatu anaamua kutengeneza yak wake. Mbaya zaidi hata yale ambayo hayafahamu atataka kufanya mwenyewe ikiwamo kuandika script! Trust me, wasanii hawa hawa waliopo kama wanapata tight script; mwenyewe utashangaa! Tatizo ni kwamba, wao wanafanya biashara lakini mtu ukimwambia angalau atoe 1 million kwa script, ataona nyingi!