Kwa wale wahenga ambao tulikutananna harakati za Mchina kuingia kwenye soko laa kuuza visimbusi vyake basi tutakuwa tunakumbuka namna ambavyo Kampuni ya StarTimes ilivyoingia nchini. Mwaka 2009 mpaka 2010 wakati watoto Wa Madiba wapo busy kuandaa michuano ya Kombe la Dunia.
Basi StarTimes naye akaingia kumpa presha DSTV maana ujio wa kombe la Dunia ndani ya bara la Afrika ulifungua fursa kibao za kibiashara na kijamii. Waliokuwa na macho ya kutazama fursa walipiga pesa ile mbaya.
Enzi hizo visimbusi vyote vilikuwa na offa za ajabu sana huku maafisa mauzo wakihaha huku na kule kutafuta na kuwashawishi wanunue visimbusi hivi huku kukiwa na offa za miezi ya bure, wale maafisa mauzo walikuwa wanapigwa vumbi ile mbaya ili Mchina apate hela.
Kama kawaida ya Mchina, yeye alipoona soko la luninga za chogo zimeanza kupoteana akatuletea visimbusi ndani ya TV bhana. Huku akiendelea kupiga pesa na promosheni na offa lukuki.
Mitaani walitengeneza mabanda maalumu ya Mauzo, wanafunga Antenna zao na kuweka luninga zao, tulikuwa tunatazama movie bure bure kitaa, huku tukipewa vipeperushi tupeleke nyumbani ili Mshua apate kununua aidha kisimbusi ama kununua luninga yenye kisimbusi.
Sasa ndani ya Channel za StarTimes kulikuwa na channel moja hivi ya kipekee sana, achana na hizo
KidsCo ama
Nickelodeon hapana, kulikuwa Na channel kwa jina la
Foot School TV nadhani hii ndio inabakia kuwa channel bora ya michezo kwa watoto kuwahi kurushwa na StarTimes mpaka sasa.
Wakati mchana unapofika tu, Foot School TV ilibadilika kuunganishwa na vituk vya michezo kutoka vilabu vya Liverpool pamoja na AC Milan, tulizoea kuziona kama Liverpool TV pamoja na AC Milan TV, wakati ule unakutana na vipindi moto moto sana.
Footschool TV kulikuwa na mahojiano pamoja na best moments zilizotokea viwanjani. Ilikuwa kawaida kuwaona watu kama
Paolo Maldini na kina
Steven Gerrard wakiwa wakifundisha dunia sanaa na sayansi ya kucheza mpira.
Lakini utamu haukuishia hapo tu! Chaneli hii ilitenga muda maalum wa kuchambua malezi na ubora wa academy kubwa za soka duniani. Tulionyeshwa jinsi madogo janja wa
La Masia,
Ajax, na
Manchester United walivyokuwa wakifundishwa kupiga pasi mshono na michezo yao bora.
Kusema ukweli, baada ya kutazama La Masia kwa saa mbili hivi, kila mtoto mtaani alianza kujiona kama fundi wa soka—hata kama mpira wenyewe ulikuwa wa sembo! Ni Footschool TV ndio ilitufundisha kuhusu watu kama
Abdou Kader "Titi" Kone pamoja na
Benjamin John.
Picha lilikuwa linaanza siku ya Jumamosi asubuhi. Kabla hata haujamaliza usafi mzee baba, tayari uko mbele ya TV ukiwasubiri ma-maestro na mafundi wa freestyle:
Abdou Kader "Titi" Kone na
Benjamin John.
Wawili hawa walikuwa wakifanya mambo ya ajabu sana na mpira kwenye kipindi maalum cha
dribbling na
freestyle. Walikuwa wakizungusha mpira shingoni na mgongoni kana kwamba una sumaku na mara kadhaa walikuwa Wakirekodiwa wanafanya hivi mitaani.
Katika kipindi cha ujio wa Kombe la Dunia la 2010 huko Afrika Kusini,
StarTimes iliandika historia kubwa kupitia chaneli hii. Foot School TV ilionekana kwenye
Channel 250 pamoja na 252 kwa visimbusi vyake na huku baadaye ikipatikana pia kwenye
Zuku TV kupitia Channel 650.
StarTimes walileta ladha tofauti ya soka la dunia moja kwa moja kwenye sebule zetu. Kwa vijana wa enzi hizo,
Foot School TV haikuwa chaneli tu—ilikuwa alama ya burudani, ufundi, na mwanzo wa mapinduzi ya utangazaji wa soka barani Afrika. Na hadi leo, hakuna chaneli iliyowahi kufikia kiwango kile cha aura.
Foot School TV ilianzishwa na kampuni ya Premium2Home kutoka Luxembourg mwaka 2003 na mwaka 2013 channeli hii iliacha kufanya kazi baada ya kampuni kusitisha urushwaji wa matangazo yake.