Footballer ataka kuvunja ndoa ya Jay Dee na Gardner?

Footballer ataka kuvunja ndoa ya Jay Dee na Gardner?

Fareed

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2010
Posts
328
Reaction score
135
Baada ya kuwapa michapo ya ukumbi wa disco raining money courtesy of Hasheem Thabeet, sasa nawapa vimbwanga vya masupa staa wengine wa Bongo.

Hawa ni muimbaji Lady JayDee au "Jide" na mume wake, mtangazaji wa zamani wa Redio Clouds, Gardner G. Habash. Lady Jaydee ni muimbaji wa bendi ya Machozi na anaendesha ukumbi wa starehe wa Nyumbani Lounge ulio nyuma ya Best Bite pale jijini Dar.

Ilikuwa ni usiku wa Jumapili, Mei 29, 2011. Credo Mwaipopo anayecheza mpira nchini Sweden alienda Nyumbani Lounge na rafiki yake aitwaye Pacha. Jide alivyomuona Mwaipopo alimrukia na kuanza kumkumbatia. Wakakaa kwa karibu huku Mwaipopo akiwa anamshika kiuno Jide, kwa mujibu wa mashuhuda. Inadaiwa kuwa Jide na Mwaipopo wana urafiki wa karibu kwa muda mrefu. Hata Jide huwa anatoa habari za kumhusu Mwaipopo mara kwa mara kupitia blogu yake, kama habari hii ambayo amewahi kuitoa Jide kuhusu rafiki yake huyo:

Lady Jay Dee: CREDO MWAIPOPO AMEUMIA MGUU

Wapasha stori wanasema ghafla Gardner alitokea na kuanza kuhamisha hasira zake kwa Pacha. Inadaiwa kuwa Pacha aliagiza redbull na maji, Gardner akamwambia leta elfu 10 kama kumkomoa. Pacha akakataa na kumuita mhudumu akamwambia vinywaji hivyo ni shilingi 4,500 tu.
Hapo basi Gardner akaanza kumrushia maneno Pacha na kumtemea mate. Pacha akamjibu kwa kumtemea mate pia. Ukaanza ugomvi, ambapo Mwaipopo na Pacha wakaamua kuondoka kwenda Maisha Club huko Masaki.

Hivyo basi Gardner akawasha gari aina ya Nissan Murano ya mke wake Jide na kuamua kuwafata kina Mwaipopo mpaka Maisha Club. Wakiwa nje ya Maisha Club, Gardner alimfuata Pacha na kuanza kupigana naye hapo nje ya parking ya club hiyo.

Pacha akamwambia Gardner najua tatizo lako ni kuwa Mwaipopo anakula mzigo kwa Jide (yaani wana uhusiano wa mapenzi). Hapo Jide naye akashuka kwenye gari na kumwambia Mwaipopo aache unafiki.

"******** zenu, mnataka kuniulia mume wangu? Mnajua umuhimu wake kwangu?" Alisikika Jide akisema baada ya Pacha kutoa sime na kumtishia Gardner.

Mtu mmoja aliyeingilia kati ugomvi akakatwa na sime shingoni lakini inasemekana hakuumia sana japo damu zilitoka.

Jide, ambaye anasifika kuwa ni mvutaji mzuri wa majani (weed), naye anasemekana mara nyingi hugombana na wasichana wanaoenda hapo Nyumbani Lounge kuwashutumu wanatembea na mume wake.
 
Kwa mimi sio fun kabisa wa Jide na huyo mumewe anaonekana yupo desperate na anampendea pesa mkewe wote mfwuuuuuu
 
Umeacha biashara yako ya saluni pale kwa tumbo tandale? Maana wateja wako wanakuulizia.
 
JD kwa majani ameshindikana mbona inajulikanaaa!!!!!ila GGH amemsaidia sana kufika hapo alipo maana kwa jinsi alivyo angekuwa anahonga sana ili awe naoo wasikimbie
 
Jide anakula jani? i am so disappointed!nilikuwa namuona kama ni staa mmoja composed mambo yake hayapo mitaani!
 
Jide anakula jani? i am so disappointed!nilikuwa namuona kama ni staa mmoja composed mambo yake hayapo mitaani!

Oyaa kula nyasi mbona kitu cha kawaida sana, ukijua listi kamili mbona ndio utapagawa kabisa.
 
km ni kweli basi hiyo nyumbani lounge maisha yake ni mafupi saaaana hiyo gombana gombana na wateja si nzuri kabisa kuna kuwa hakuna descipline so watu wataanza kukimbia.
 
Au ndo maana Jide alisema amekuwa teja wa weed na malovee. Sasa inakuwaje tena Gadner amvamie Pacha badala ya Credo mla zigo.?
 
km ni kweli basi hiyo nyumbani lounge maisha yake ni mafupi saaaana hiyo gombana gombana na wateja si nzuri kabisa kuna kuwa hakuna descipline so watu wataanza kukimbia.
Hata Machozi bar aliyomiliki pale Sinza haikufanya vizuri kutokana na mambo ka hayo bora abaki kuwa muimbaji tu na kupokea mshiko
 
Hela mbaya sana hasa kama huna cha kuifanyia. Habash ana tabu kubwa, na hivi alinuia wanawake mchacho kwake ni laana, basi wenye fweza ndo hao.
 
Msimamo wangu siku zote ni

(1) Marufuku kumfuatilia (simu, facebook, emails etc) mwenza wangu.
(2) Marufuku kupigana au kumtukana mtu anaetembea na mwenza wangu, hata kama niwafumania live, maana huyo mtu haibi kifurushi/mzigo, bali mtu mwenye akili timamu na mwenye uwezo wa kukubalia au kukataa uhusiano wowote na mtu yeyote.

Hapo G na JD wote wamejiaibisha kama kweli walihusika ktk sakata hilo. Wao ni watu wazima, they should have done better than this, yaani vijana wa shule wagombanie wapenzi na watu wazima pia, tena wenye exposure na mambo ya maisha yanavyoenda?

Hayo yalikuwa mambo ya kuyamaliza nyumbani, afterall, celebrity kukumbatiwa ni kawaida sana tu.
 
Back
Top Bottom