Kuna mambo mengi yanayoaminika sana katika jamii zetu na huwapa watu mashaka. Nimejaribu kuweka hii list. Naamini wengine wataongezea.
Kuhusu mambo ya uzazi:
1. Wazazi wakifanya tendo la ndoa mtoto anapata madhara (maziwa yanachacha)
2. Mapacha wakirukwa wanakufa (endapo mzazi mmoja atafanya ngono nje ya ndoa kabla au baada ya kuzaliwa)
3. Wazazi wakifanya ngono nje ya ndoa wanambemenda mtoto
4. Baba akimpiga mtoto kichwani na uume wake mtoto anakufa
5. Mama akimlaani mtoto wake kwa kumwonyesha sehemu nyeti anakuwa kichaa
6. Ukitembea na ndugu yako wa damu watoto wanaozaliwa wanakuwa mazezeta
7. Ukifanya tendo la ndoa na mama mja mzito (karibia na kujifungua) mtoto anazaliwa na uchafu kichwani.
8. Bundi akilia karibu na nyumba basi lazimi kuna mtu atakufa kwenye familia hiyo
9. Mwanamume akitembea na mtu na mwanaye anakuwa na uwezo wa ajabu. Mfano, akitemea mate siafu wanatawanyika na kupoteza dira
10. Ukipanda nevu ya mwanamke (kwa wale wenye ndevu) utafanikiwa kwenye biashara na kuwa tajiri mkubwa sana.
11. Kuna mbegu za mimea fulani na mkia wa ndege fulani ukigusisha kwenye mkojo wa mwanamke basi atakutafuta kwa udi na uvumba (ni dawa ya mapezi)
12. Ndoa, siku ya harusi lazima mwanamume ahakikishe anamkanyaga kidole cha mguu mwanamke, akimuacha mwanamke akamkanyaga yeye, mwanamke atamuendesha kwenye ndoa yao
13. marufuku kutwanga usiku kwa sababu wachawi watakuja na pia aliamini kwamba
14. mtu haruhusiwi kufagia usiku kwa kuwa ataita wachawi na haruhusiwi kununua au kuomba chumvi usiku. akihitaji aseme anaomba 'dawa
15. Ukimwimbia mtu chupi au nywele za sehemu za siri (kwa wanawake) basi unaweza kumfunga uzazi.
16. Ukinyoa nywele lazima uzizike ardhini vinegenvyo wachawi wakiziokota watakuua.
17. n.k.....
Kuhusu mambo ya watoto
1. Kuna baadhi ya watu hawatakiwi kumwona mtoto mchanga kabla ya kitovu kudondoka kwa hofu kuwa anaweza kufa au kudhurika. Kwa hiyo inabidi mtoto afichwe
2. Kitovu kikidondokea dudu ya mtoto (uume kwa mtoto wa kiume) anakuwa ******* (hawezi kuzaa)
3. Kitovu kikidondoka lazima kitunzwe vinginevyo mtoto anaweza kufanyiwa mambo ya uchawi endapo walozi watakiokota
4. Kitovu anafungwa mtoto kiunoni ili asipate mchango (basically ni utapiamlo)
5. Kuna dawa lazima mototo afungwe kiunonni au kwenye mkono ili asipate mchango.
6. Mtoto asipopelekwa kwa babu zake atakuwa anapata ndoto za ajabu na kustuka stuka usiku. Lazima wazee wamwone, wamwekee mikono na baadhi ya makabila wampatie na jina.
7. mtoto akizaliwa lakini akiwa analia sana labda nyumba haijamkaribisha........mzee wake apige hodi kila kona ya nyumba!
8. Mtoto lazima apewe jina la utoto (la ukoo) na la ukubwani (may be la dini)
9. N.K
Nitaendelea kuongeza na nyingine nikizikumbuka. Pia wengine wanaweza kuongezea kutoka kwenye makabila yao.
Kweli kuna umuhimu wa kuweka hivi vitu kwenye kumbukumbu. Vijana kama mdogo wangu Teamo watayahitaji haya mambo muda si mrefu.