Force account ni mfumo wa upigaji, nafananisha na upigaji wa mabilioni ya JK

Kama ndio mfumo ulio bora waambieni CRB wafute makampuni ya Ujenzi .
Force Account umeharibu mzunguko wa fedha mtaani na kusababisha makampuni mengi ya ushauri na ujenzi kujifunga yenyewe.
Kwa ufupi ni mfumo ambao haufai hata kidogo kwa kuwa athali zake ni nyingi kuliko faida mfano Graduates wengi wako mtaani na wale walioko masomoni hawapati mentors wa kuwafundisha kazi kwa vitendo/field kazi nyingi zinafanywa na mafundi bila weledi /usimamizi mathubuti.
 
Tuelimishe Force Account inafanyaje kazi?

Amandla...
 
Chief pamoja na andiko zuri, ila nafikiri hufahamu vizuri mfumo wa force account. Madhaifu unayoyataja yanaweza kutokea pale ambapo hapana usimamamizi mzuri. Huu mfumo una ufanisi mkubwa sana tofauti na mfumo wa wakandarasi. Labda toeni mapendekezo ya nini kiboreshwe
 
Ulichosema ndo ukweli ni mfumo bora wa kubana matumizi kuliko kutumia wakandarasi wenye gharama kubwa hata kwa kazi ndogo tu ya kujenga choo.
 
Nakubaliana na wewe 100%, huu mfumo unachohitaji ni usimamizi mzuri ila unaokoa mamillion ya pesa ambayo yangekuwa wasted.
 


Hebu elezea Basi uzuri wake ukilinganisha na ule wa awali @ Kidonge!
 
I agree with you. Mfano (Ila pia ubora utasimamiwa na nani kwenye halmashauri? ) .... Natumaini ipo KAMATI YA USIMAMIZI ambayo inajumuisha wataalamu wa Halmashauri i.e. Archtitects, Engineers, Economists e.t.c
 
Hivi hapa mnaongelea nini? Yani mmeniacha kwenye mataa ni kama mnajadiliana stories mnazozifahamu wenyewe. Ngoja niende zangu kusaka mada za Mbususu.
 
Ungetoa detailed analysis juu ya ubora wa mfumo siyo kusema tu bi bora wasiojua kuwa ni bora watajuaje ?

Au kwa sababu mnanufaika nao ni bora kwenu ?
 
Tegemeeni Ester luxury Coach za Singida- Dar kuongezeka
 
Hii ya kugawanya shs 12,500,000= kwa kila darasa unahitaji ukiritimba wa nini? Ni kuwaita wananchi wadau wa shule kwenye mkutano na kuwambia tumewakabidhi viongozi wenu hii fedha kiasi kadhaa hakikisheni mnaliona darasa na watoto wenu wanasoma, kwisha.
 
Nakubaliana na wewe 100%, huu mfumo unachohitaji ni usimamizi mzuri ila unaokoa mamillion ya pesa ambayo yangekuwa wasted.
Nafikri hatujamwelewa mtoa mada yeye hoja yake haijalenga unafuu wa mifumo ila umelenga security na ubora wa kinachopelekwa huko mwisho.

Inasikitisha unausifia mfumo ila umeanza kwa qualification ya hoja yako.

Maana yake mfumo unamapungufu ya usimamizi.

Umeliona hilo la usimamizi je akiwepo msimamizi asiye na maadili ya kazi yake inakuwaje?

Nieleweshe kidogo
 
Mfumo huo umekuwa ukitumika kwa zaid ya miaka sita na umeleta tija kwa miradi mikubwa kutekelezwa kwa bajeti ndogo. Tofauti na umpe mkandarasi..pia wanavijiji kunafaika moja kwa moja. Mhandis wa halmashaur ndiye anayesimamia.. manufaa ni makubwa kuliko changmoto
 
Pesa ziende kulekule kwenye akaunti ya shule na ziidhinishwe hatua kwa hatua kutegemea na hatua za ujenzi, baada ya wakaguzi kujiridhisha kwa kila hatua.....
 
Tunajadili kuchukua bilions of money tuzisambaze kila kata au sijawaelewa?
 
Mfumo ni mzuri. Sasa changamoto unakipa Kijiji Mil 200 halafu hizo kamati za wanakijiji hakuna mtaalam wa manunuzi, hakuna mtaalam wa ujenzi, hakuna mtaalam wa account n.k. Mapungufu yanakuwa makubwa Sana.
Kuna Halmshauri zina wataalam wa ujenzi watatu halafu kuna miradi zaidi ya 30 ndani ya Halmshauri Kwa wakati mmoja halafu ufikaji wa baadhi ya sehemu ni Shida hasa hasa Halmshauri za wilaya. Wenye mamlaka waangalie hili.
 
Hata wewe hapa unalaumu. Ni vyema ukaeleza faida za mfumo huu ili kutoa elimu kwa umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…