ndio umuhimu wa kuwa na hivyo vitu huku maana vinatia hamasa. Mimi binafsi haya magorofa ya Nairobi ndio yalinifanya nipige moyo konde na kuamua kutia bidii ndani ya maisha. Siku moja, miaka ya hapo awali nikiwa dogo, nilikua nimetulia pale bustani ya Uhuru park, maeneo ya juu karibu na community, ambapo ukiwa hapo unapata picha nzima ya magorofa ya Nairobi.
Nikaanza kujiuliza maswali mengi sana, hivi haya magorofa ni kwa ajili ya nani, mbona nisiwepo humo pia, umuhimu wangu kwenye maisha ni nini, miundo mbinu hii ipo kumnufaisha nani, waliopo humo wana nini zaidi yangu, haja gani ya kuishi kwa mazoea....nilijiuliza maswali karibia mia hivi.
Hapo nikafanya maamuzi yaani lazima nitoke kimaisha, KWA HERI AU KWA SHARI.... nikaanza kupambana bila kupoteza wakati, nikasomea kila nilichokutana nacho, nikabadilisha aina nyingi za ajira...... Hivyo kifupi, tunahitaji hayo mavitu humu.