Ford Nyeupe - Ubungo Intersection to Sam Nujoma Road

Ford Nyeupe - Ubungo Intersection to Sam Nujoma Road

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,379
Reaction score
41,294
Hamjambo wajukuu,

Mambo ni mengi muda hautoshi basi alfu lela ulela kibao...

Sikuwa na mpango wa kutoka leo, maana jua kali halafu usingizi ulikuwa bado umeshika hatamu.
(Usijiulize maswali mengi, niko naiti shifti sikuhizi). Waja si watu wazuri wanataka niache kazi ili nidange, waaapiii sikubali ng’oooo nilivyo mbishii.

Basi bana huku nagaa gaa kwenye mkeka kibarazani mbagala majimatitu simu ikaingia...

Bi Kasindee njooo, niniiii njoo bwana nimekuhamu....! Khaaa sasa si unifate..!??? Oooh unajua nakuitia dolariii.....!🤑🤑🤑

Weeeh macho yakanitoka kodooo nikajiswafi mbiooo dera tumboni ndani ya bajaji.

Nikajiuliza napita njia ipi niwahi dolari maana tozo kila kona na nshapewa muda nikichelewa dolari 💸 zinaota mbawa.

Nikajistukia nimefika Ubungo intesekesheni na lokesheni ni maili kadhaa mbele.

Sasa Ford nyeupe imekujaje, yuko nyuma yangu anaonekana ana mambio kama yote halafu mie ndo nauanza mlima wa intaseksheni.
Nikajisemea mi mwenyewe nna haraka ila bajaji haiendi nguvu ndogo sikupishi ukitaka tafuta upenyo wa kuovateki.

Tulivyoanza kushuka kuingia SamNujoma bajaji ikapata nguvu nikachochea moto weeeh kumbe Ford kakasirika...😅😅😅

Baada ya kumaliza intaseksheni akapata upenyo wa kunipita kaniangalia hanioni fulu tinted 😝😝😝

Mbele kidogo sijui kakwama wapi nikampita baadae nae akanipita nikasemaa okeeee unataka ligi na bi K’....

Basi nikajamkuta Ford nyeupe namba C anasubiri kuingia barabara ya Sinza mie taa zimeruhusu yuleeee nikawahi dolari zangu Mikomiko.

Habari inahusu ninii.....?
 
Dah[emoji848][emoji848]..sitaki kuamini ukilaza ndy unanianza ,sijatoka hata na kimoja
 
Kasie ukitaka ligi ingia barabara ya Kimara <> Kibaha...huko Ubungo utaishia kuparamia madaladala ya Ubungo Kawe
 
Hiyo bajaji ulikuwa una drive wewe huyu?

Sijawahi ona mdada anaendesha hizo motorcycle mie
 
Siku hzi Kuna k vant feki Ni hatari kwa afya

Ijumaa usiku walitutengenezea cocktail wakasema wameweka gin na whiskey kumbe Vant na Valuu...!

Sina hamu...🥵
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Kasie ukitaka ligi ingia barabara ya Kimara <> Kibaha...huko Ubungo utaishia kuparamia madaladala ya Ubungo Kawe

Shugaaa ile barabara na hii bajaji natafuta kutoa mchozi tuu....🤪

Lami imenyooka laini tamuuu, kuitendea haki yafaa niwe kwenye gari sio usafiri.

Hapo naweza peleka ligi hadi mtu akatamani kumuona dereva ni nani....🤪.

Kasie Mavurugu 😊.
 
Nimeshindwa kuelewa sijui ni kwasababu nimepiga k vant nitajaribu kuupitia tena nikiwa sijautwika
 
Back
Top Bottom