mama dunia
JF-Expert Member
- Dec 22, 2011
- 420
- 84
Yaani jana nilikuwa natizama citizen tv ya kenya, Raila Odinga akifungua kiwanda kipya cha bia huko mombasa, sasa nilijisikia kutahayari pale aliposema 'namkoti' kwa kiswahili, "Nchi yoyote haiwezi kuendelea kwa kutegemea wawekezaji wa nje" akimaanisha kuwa wawekezaji wa ndani ndo mambo yote.... kweli nilitahayari kwakuwa mie hapa bongo nimezoea kusikia kila kukicha kuwa wawekezaji hao wa nje ndo wanaoleta maendeleo nchini, na wamekuwa wakija na kualikwa na kutembelewa kila sikuuuu... sasa sielewi lipi ni lipi
Na upuuzi wenyewe unaanzia pale airport. Wageni hawasumbuliwi wala kuulizwa maswali ya kijinga, lakini ukiwa na passport y kibongo basi miswali ya kijinga kibao. eti mara "ooh unafanya nini huko nje?" Mbona umebeba miswaki miwili? Mbona una viatu vingi?Yaani jana nilikuwa natizama citizen tv ya kenya, Raila Odinga akifungua kiwanda kipya cha bia huko mombasa, sasa nilijisikia kutahayari pale aliposema 'namkoti' kwa kiswahili, "Nchi yoyote haiwezi kuendelea kwa kutegemea wawekezaji wa nje" akimaanisha kuwa wawekezaji wa ndani ndo mambo yote.... kweli nilitahayari kwakuwa mie hapa bongo nimezoea kusikia kila kukicha kuwa wawekezaji hao wa nje ndo wanaoleta maendeleo nchini, na wamekuwa wakija na kualikwa na kutembelewa kila sikuuuu... sasa sielewi lipi ni lipi
Wakuu Tatizo liko kwa Wabongo wenyewe na si kwa hao wawekezaji, pamoja na Rushwa tukubali hawa wazungu wan mitaji mukubwa sana ukilinganisha na wazawa,
Wazawa kama wangeacha ubinafisi na kuunganisha Nguvu tungeweza kupambana na wazungu na kuwashinda, chukulia mfano wa Supermarket za Shoprite, watanzania walikuwa na uwezo wa kushindana na hawa makubulu lakini tatizo kila mmoja anataka awe na ki minsupermarket chake sasa hii wapi na wapi?
Njoo kwa kampuni za Ujenzi, Makandarasi wakibongo kama wangeweza kuungana na hata makandarasi 20 na kuwa na kampuni moja nina uhakika wangeweza kushindana na wachina na watu wengine, tatizo kila mmoja anataka aonekane anaweza na ana kampuni
Kama watanzania hawataunganisha nguvu tutabakia kulalamika tu, leo MZUZU nataka watu wakufanya nae kazi, najua watu wengi wataona ni bora wange kuwa pekee yao, so ni lazima tunao lalamika tuonyeshe mfano
So mnao lalamika pls anazeni kwa kuonyesha mfano wa kuunganisha nguvu na kuja na kampuni moja ya kueleweka na si kuwa na utitili wa kampuni