Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nakuhakikishia mkuu utatembea wewe. Utataka kila mtu awe rafiki yako. Utawafanyia biashara wamerakani mpaka uchoke. Wewe ni afisa masoko usiyelipwa. Ni kazi ngumu sana kupata faida huko. Nakushauri fikiria kingine. Wenzako tulishatoka hUko miaka mingi.wanaJF nataka kujiunga na huu mtandao wa biashara katika forever living products. Tueleweshane nini kilichopo ndani kwa wale wajuzi
Shida ni mtaji au ni nini best,why dont u kujiuzia bidhaa zako mwenyewe utakazo na si kuchaguliwa.Be creative na anzisha chako.
Mkuu ebu nijuze sababu hasa zilizokuondoa huko wewenakuhakikishia mkuu utatembea wewe. Utataka kila mtu awe rafiki yako. Utawafanyia biashara wamerakani mpaka uchoke. Wewe ni afisa masoko usiyelipwa. Ni kazi ngumu sana kupata faida huko. Nakushauri fikiria kingine. Wenzako tulishatoka hUko miaka mingi.
Wale waliongia mwanzoni na kujenga mitandao ndiyo walipata fedha. Ni biashara inayowafaidisha watu wachache walioko juu majority mnabakia kuwa watu wa kuwaandalia maisha watu wengine. Kwanza unatakiwa uwe na Kundi la watu wengi wachakalikaji kwa maana na kuwa na uwezo wa kuingiza watu wengi na kisha Kundi hilo la watu wako liwe la watu wenye fedha na wewe mwenyewe uwe unanunua virutunisho hivyo na kuvitumia mwenyewe kwa wingi. Na lazima uwe chinga fully ukitembeza mitaani au uwe na duka la dawa linaloeleweka huku ukiwakonvice watu. Wanunue kwako na wajiunge na mtandao huo. Mimi nilishindwa, na ninaposhindwa JAMBO huwa nashindwa kweli kweli na silirudii tena. Kwa hiyo maelezo nitakayekupa hapa ni ya kushindwa tu maana nimeona watu wanazeeka na hizo forever na GLND wakiwa masikini. Labda tafuta mtu aliyefanikiwa ndugu yangu atakutia moyo. Mimi sitaki hata kuisikia hiyo forever. Kuna jamaa nilimwambia asijiunge hakunisikia sasa mwenyewe ameachia ngazi. Epuka kupoteza muda wako kwa kuwafanyia kazi watu. Fanya vitu vya maana. Hii ni technic know how and know what tu, hata wewe unaweza kutumia kupata vibarua ambao wachache Kati yao utawalipa vizuri ili wakutangazie sifa njema kwa biashara yako while majority are crying. Sina maelezo mengine tena zaidi.Mkuu ebu nijuze sababu hasa zilizokuondoa huko wewe