Jamani tusifarijiane tukaja danganyika kirahisi. Mpaka sasa hakuna dawa yenye uwezo wa kuondoa VVU kwa mtu aliye athirika. Hii ni kutokana na tabia ya VVU ambavyo ni virusi vilivyo kwenye kundi la RETROVIRUS.
Virusi hawa kwanza wanauwezo mkubwa sana wa kujibadilishabadilisha, kiasi cha kwamba ndani ya mwili wa mtu mmoja kunakuwa na aina tofautitofauti ya virusi hawa ( Kitaalamu Quasy species)(strains). Hii hufanya kinga ya mwili kushindwa kuwaondoa.
Pia virusi hivi huathiri seli zinazohusika na kinga mwilini zenye kitambulishi cha CD4, kama CD4 +ve T-Lymphocytes, Macrophages(monocytes), na Dendritic cells. Ndani ya hizi seli kirusi hiki huweza kukaa kwa miaka mingi wakiwa katika hali ya utulivu i.e. latent state. Na dawa haiwezi kuja kuwaua hawa virusi ndani ya hizi seli bila kuziua hizi seli , kitu ambacho ni hatari kwa afya ya muathirika.
Hawa virusi wanazaliana ndani ya hizi seli zinazohusika na kinga ya mwili na ili kutoa virusi wapya hizi seli hufa. na ndo maana kiwango cha CD4 seli ndani ya mwili hupungua.
Kilichowezekana sasa ni kupunguza kasi ya kuzaliana kwa hawa virusi ndani ya mwili na hivyo kupunguza kasi ya kuuwawa kwa CD4 +ve seli na hatimaye kupandisha kinga ya mwili. Ila seli zilizo athirika zitaendelea kuwa na virusi bali watakuwa hawazaliani.
Tuendelee kumuomba mungu tafiti zinaendelea kufanyika ili tuweze kupata kinga mbadala ya VVU/UKIMWI.
Mpaka sasa kinga pekee madhubuti ya ukimwi ambayo itakupunguzia uwezekano wa kupata VVU/UKIMWI kwa asilimia kubwa sana ni abstainace from having unprotected penetrative sex with multiple patners.