Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.

Tutakutana mbele ya safari, Nipo namalizia chapter ya pili hapa. Vipi mzee kule kwa wazee wenzangu unapatelekeza ama ngoma ni mwendo wa parallel execution.
 
Reactions: MC7
Swali la kizushi, Wewe hilo group nani alikuingiza ama alikukaribisha.? limeanzishwa lini/Ama lini wewe umefahamu uwepo wake.? Nini kimekuashiria kuwa hao wawili ni matapeli.?
Swali juu ya swali jibu swali ulilo ulizwa au unaonaje mkuu maana sisi watanzania hatuna uzoefu hii biashara sasa inapotokea mtu kauliza swali la manufaa kwa watanzania na wewe unakuwa mkali unatia ukakasi katika nia yako.
 
Very educative and inspiring thread kaka..kudos for real...if there is stil vacant to attend the training please count me in...all the best kwenye maandalizi na team yako, this is awesome thread
 
Reactions: MC7
Mkuu link ya kujiunga na hili group iliwekwa humu, kila mtu akiuliza kama kuna group la WhatsApp Jamaa wanaweka link Yao. Ni matapeli tu


Hiki kitu hakina shortcut wadau, Ni lazima usome+kufundishwa ndo ufaidike na forex, Hili ni angalizo ambalo wadau wazoefu wamekuwa wakilitoa toka thread inaanza. Sasa ambao wanakimbilia huko whatsapp ni wanaotaka shortcut, na nachelea kusema wakitapeliwa watakuwa wamejitakia wenyewe. Na kama umesoma, ukakumbwa na ugumu ukiuliza humu, wadau kama bavaria na ontario wamekuwa wepesi kujibu. Why mkimbilie whatsapp.?

Ila tuu, angalizo, Tusitegemee kukusanya ambapo hatukutawanya. Ontario keshawaambia yeye alsoma vitabu 6 na ndo yupo hapo alipo, na bado hajaimaster vyema mpaka anahost toka nje trainners kuja kufundisha
 
Thread nzur mkuu but we need a training kama ulivyosema hapo mwanzon kipind niko chuo a was interested na somo moja linaitwa International Finance lilinipa mwanga sana kuhusu Forex but am very ready for the training bro.
bosi hujasoma IFM kweli cz pale kuna International Finance, International Trade, International Banking Operations, Treasury Management na Corporate Finance katika course ya Bachelor of Banking and Finance na kuna walimu nondo sana kama Dk. Doriye, Dk. Abdul Nkoba (sikumbuki jina lake vzr) na to be Dk. Mwambuli etc etc ukitulia vzr haya mambo pia yalipigwa hapo chuo sema kwa level ya kukufanya uelewe ni nn hichi na sio uapply ww katika mazingira yetu!!!
 
Swali juu ya swali jibu swali ulilo ulizwa au unaonaje mkuu maana sisi watanzania hatuna uzoefu hii biashara sasa inapotokea mtu kauliza swali la manufaa kwa watanzania na wewe unakuwa mkali unatia ukakasi katika nia yako.

Brother ni swali gani nimeulizwa sijalijibu.?
 
Achana na story za figisufigisu..huo ni uongo wa mchana kweupe..
Forex yenyewe siyo kwamba unaenda kujichotea tu mahela, ni kama kamari tu tena wanakwambia "losses can exceed your deposits" kabla hata hujajiunga!
Mabenki hayana huo muda wa kukuzuia wewe eti usiijue forex
 
Brother ni swali gani nimeulizwa sijalijibu.?

Mimi nilikuuliza utaratibu wa kuanza kutusajili kwenye hiyo list ya 300 au zaidi, Na kutaka kukupa ushirikiano ili zoezi liende haraka. Lkn sijapata jibu mpaka sasa.
 
Kumbe wewe mwalimu wa primary!
Sasa kwanini huwa unajitoa fahamu kule jukwaa la siasa
 
Tulizeni mishono jamani hatujui hata Antario atatumia vigezo gani kupata hao 300 wa mwanzo. The best way is be patient tule masomo ya hicho kitabu elekezi huenda ndo ticket yenyewe ya kuingia kwenye top 300 huku tukisubiri a way foward toka kwa kijana wetu.
 
Mimi nilikuuliza utaratibu wa kuanza kutusajili kwenye hiyo list ya 300 au zaidi, Na kutaka kukupa ushirikiano ili zoezi liende haraka. Lkn sijapata jibu mpaka sasa.

Basi swali ulilielekeza sehemu sipo, ndo maana hukupata jibu. Maana mimi si mhusika niliyeianzisha hii program. Mimi ni mwanafunzi tuu kama wewe. Soma vizuri post za thread utamjua organiser wa hiki kitu ni nani.
 
Nilielekeza kwa Ontario, ila kukuuliza wewe nimefanya kosa. Sorry for that. Hope umenielewa.
 
Naungana na wewe hili GROUP la matapeli.. wanasema Eti kuna kampuni...!! Wapuuz hao dahhhhhh... bora lile GROUP la WhatsApp la kwanza.... wana strategy zenye akili....

Hilo la kwanza limeishia wapi?
 
Dah! Huu uzi niliuona lakini nikaupuuzia. Imenichukua masaa ma4 kusoma post yako ONTARIO pamoja na asilimia 90+ ya comments za wadau. Nimejuta kwa nini sikusoma juzi. Nimeisubscribe hii thread.. najaribu kuona kama naweza kukufollow pia.. niko mwanza. Na ninaomba kuwa miongoni mwa hao 3
 
Pili nakuomba mkuu Antario nimeona mkuu Bavaria with zero alcohol anadai kuwapa signals vijana wako ni kuwafanya wawe vilema wa kufikiri. Please chondechonde km ni ivo usitufanyie ivo mkuu wengine tunachukia sana kutafuniwa au kukaririshwa km mifumo yetu ya elimu inavyotulemaza matokeo yake umesikia humu graduates anagombania remote na mdogo wake nyumbani. Tupe shule yenye misingi ya kutufanya tuwe ambassadors wako wazuri kwa wengine na sio mategemezi km mitoto ya bata
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…