Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Note biashara ambayo nimewahi kufanya tofauti na hizo kamali hapo juu ni ufugaki kuku tena zamani sana huko j4.
kamali zipi mkuu mana hapo kamali ni moja KUBETI, halfu we jamaa inaonekana una tamaa sana na pia ulikua hutumii akili. Naunga mkono hoja ya mods kupiga lock threads zinazohusu forex maana kuna kenge hua wanadhani kule ni mteremko mwisho wa siku wakigalagazwa wanakuja kulialia humu utadhani watoto wadogo.
 
ulikua unafanyia analysis kwenye simu??
Mkuu kuhusu analysis tulikuwa tunapiga ya kufa mtu tena tulikuwa wengi tena watalaam tupu wa economics, mathematics , statistics ,Actuarial

Hakuna device ambayo tulikuwa hatuna tulikuwa tupiga kuanzaia technical, fundamental mpaka sentimental analysis kabla hatujaingia sokoni

Kuna lile jengo la udaktari pale udsm ambalo lilikuwa la madaktari tumepigisha watu sana mule seminar na jamaa yangu ambae sasa anaendelea kufanya trading yuko kwenye group kubwa sana hapa tz anasaidia newbie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nacho kushauri jaribu kucontrol hisia.

Yaani ulichokiandika tu tayari nimeshajua wewe ni mtu wa aina gani

Forex haiitaji wakurupukaji kwa akili hizo ulizonazo vipigo kwako vitakua haviishi, Maneno yako tu yanaonesha unasumu ndani yako unataka mtu wa kubishana nae japo kidogo upunguze machungu

Sasa uzi wangu unahusiana vipi na kufungwa kwa threads nyingine mkuu.







Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh hio sindio ile ya kuunguza Account. Unatega mtego bila stop loss unalala zako ukija kuamka unakutana na namba nyekundu zenye (-) kwa mbele 🤣🤣🤣🤣🤣
Si kweli mkuu!

Binafsi wakati naanza nilianza na scalping then day trading ila kwa sababu ya majukum nimejikuta nimetulia kwenye swing trading!!

Last time nlikua na position ya EURGBP nika hold kwa mwezi na siku kadhaa... Nikatoka na pips 820+!

Yan unakua huna presha ya kukaa na screen all the time, you just do analysis and open a trade,then unakua unaangalia trade yako once a day or once after two days!!

Si kazi rahisi ila ukii master utagundua kwamba is the best way of trading!

Pia Kuunguza account unaweza unguza hata ukiwa una scalp au day trade kitu kitacho kufanya usiunguze account ni UJUZI na Proper risk management na sio scalping au swing trading!
 
Nafurahi Sana forex kuwapiga hasara watu kibao walio ivamia Kama uvamimizi wa nzige... Watu waliingia kwa mihemko wakapigwa hasara za hatari.


Kwasasa Hali imetulia tuliiii, webaki wakongwe kazi zinaendelea Kama kawaida. Nawaomba nyie vijana na wapenda kufanya kila fursa mnayoisikia. Kuwa kabla ya kufanya Kitu chochote fanyeni uchunguzi wa kina.


Nina amini mpaka 2021 forex Trader wa ukweli Tanzania nzima hawatafika 100.


Asante Mungu kwa kutuondolea takataka kwenye industry yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulisomea nini ukiwa chuo? Au wewe una uzoefu au kipaji gani?
 
Sijui hata izo data umezitoa jalala lipi

Nikwambie tu kinaga ubaga forex industry hapa tz ndio kwaanza inachipukia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao watu 100 by 2021 labda unazungumzia kwenye group lako la WhatsApp

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana mnakata tamaa mapema sana, wengi waliodumu kwenye hii biashara walipata hasara, walipoteza mahusiano, walidharaulika lakini walivyoamua kukomaa na kupuuza hayo yote leo hii ndio wana enjoy na kuishi maisha wayatakayo. That's Financial freedom
 
Actuarial science mkuu



Sent using Jamii Forums mobile app
Okay. Kwa Program yako naamini unaweza kuwa Business Analyst, budget or research analyst. Kwa sasa kuna wafanya biashara wengi tu wanahitaji watu wanaoweza kuwasaidia biashara zao ziende vzuri.

Nashahuri jaribu kuangalia ni wapi watu wana changamoto za biashara za namna ya kuandaa budgets au wanaohitaji analysis ya biashara zao.

Wewe tumia ujuzi wako kuwasaidia na hapo ndipo utakuwa umejiwekea mazingira mazuri ya kupata wateja watakaokulipa fedha nyingi sana kwa kila project utakayofanya.

Kuanzisha huduma zako haichukui mwaka au miezi, ni siku utakapoamua kuanza utaanza kupata wateja tena wengi sana.

Niamini, anza leo utaona faida yake. Biashara nzuri siku zote ni ile unayotatua changamoto za watu sio lazima uuze bidhaa, anza kuuza huduma ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…