Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Baasi nikatafuta rafiki yangu alikuwa anauza karoti ilala boma kwenye meza najua wenyeji wapale wanaelewa vizuri nikwamwabia anitafutie eneo kweli akaniambia per day meza unalipia 1000 na ushuru sasa mwenye meza anataka 60k ya miezi miwili nikasema poah ,nikampatia jamaa yangu pesa .
Broo naomba msaada kuhusu hii biashara, maelekezo pliz
 
Fanya kazi kwa bidii ..money downloaders sasa hivi wamepungua sana sijui nini tatizo..
 
Tupe mwongozo namna ya kutulia ili nasisintupate kitu. Maana tunaliwa sana
Mkuu usiache betting pia labda kama hauna ujuzi nayo kuliko FX. Betting ina strategies nyingi nzuri tu watu huwa huwa wanakosea kitu kimoja tu mtu anaweka Tsh 500 anachagua timu 20 ashinde Millioni 40. Ukiangalia kwenye somo la probability hadi huo mkeka utiki kwa kweli ni bahati nasibu hapo wanaishia kumtajirisha kanjibahi. Ila ukitulia betting inalipa vizuri tu.
p
 
Mrejesho mkuu.
Ni miaka zaidi ya mitano imepita.
Nilipambana kwa njia tofauti ups and down nyingi.
Niliingia kwenye biashara ya nafaka, samaki, Nguo lakini zote zilikufa. Baada ya hapo Nikawa winga wa viatu vya mtumba karume nikawa naenda kuuza kwenye fremu yangu kawe.
Hii biashara ya viatu kwa kweli nilianza kuona mwanga na faida tena kwa haraka sana tofauti na hizo nyingine hapo juu lakini inachosha kuamka saa 8 au 9 usiku ni jambo la kawaida.
Nimekuja kufunga mwaka huu baada ya kupata ajira rasmi.
Ila kipindi hiko chote nimekuwa nikiendelea na forex pamoja na betting bila mafanikio yoyote.
Sometimes huwa natumia forex kupata pesa kidogo ya kwenda kula Bata lakini sio kama kitu cha kunivusha kimaisha.
 
Back
Top Bottom