Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Broo naomba msaada kuhusu hii biashara, maelekezo pliz
 
Fanya kazi kwa bidii ..money downloaders sasa hivi wamepungua sana sijui nini tatizo..
 
Tupe mwongozo namna ya kutulia ili nasisintupate kitu. Maana tunaliwa sana
p
 
Mrejesho mkuu.
Ni miaka zaidi ya mitano imepita.
Nilipambana kwa njia tofauti ups and down nyingi.
Niliingia kwenye biashara ya nafaka, samaki, Nguo lakini zote zilikufa. Baada ya hapo Nikawa winga wa viatu vya mtumba karume nikawa naenda kuuza kwenye fremu yangu kawe.
Hii biashara ya viatu kwa kweli nilianza kuona mwanga na faida tena kwa haraka sana tofauti na hizo nyingine hapo juu lakini inachosha kuamka saa 8 au 9 usiku ni jambo la kawaida.
Nimekuja kufunga mwaka huu baada ya kupata ajira rasmi.
Ila kipindi hiko chote nimekuwa nikiendelea na forex pamoja na betting bila mafanikio yoyote.
Sometimes huwa natumia forex kupata pesa kidogo ya kwenda kula Bata lakini sio kama kitu cha kunivusha kimaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…