Ndio wanapiga sema ni ya moto sanaa! Mi bado sijafanikiwa napata hela za mboga tu,ila pia huwa napigwa.
Kwa ufupi forex tunatabiri mwelekeo wa soko la fedha kama wafanyavyo watabiri mipira.
Sema Huku mambo Yako advanced sanaa. Kutabiri mwelekeo wa sarafu soko linafunguliwa jumapili usiku Hadi ijumaa usiku, na weekend Kuna assets zinaitwa indices hizo Haina Cha weekend.
Ukitabiri soko litapanda , unabuy ukitabiri soko litashuka unasell, so unapata faida both ups and down movements.
Elimu ya Huku ni lazima mwisho wa siku ikuoneshe mwelekeo wa soko upon wapi ndo utapiga hela.
Wingi wa pesa unaseti mwenyewe kwa tool Moja inaitwa lot size the more unaweka kubwa the more pesa inaonhezeka na loss vivyo hivyo.
pesa unapokea kupitia banks,au Skrill au Bitcoin wallet au mitandao ya simu.
Kwenye forex hatununui sarafu kama wengi wasemavyo Huku tunabashiri mienendo ya bei ama price ya sarafu, so utatabiri either soko liende juu au chini.
Soko tunabeti ama kubashiri kupitia kwa brokers kama vile templerfx,hotforex,deriv,exness na wengine wengi.
Mtaji wa kuanzia nao ni Dola kumi tu sawa na TSH 25,000/= na app tunayotumia kuzalisha na kupoteza pesa inaitwa MT4,MT5 na tovuti tunayotumia kufanyia upembuzi ama uchambuzi ni tradingview IPO google tu.
Kama wewe ni mgeni kabisa hujui pa kuanzia Anza kusoma forex kwa lugha ya kiswahili YouTube Kuna series nzuri search scalpkingfx tazama video ya kwanza Hadi sehemu ya mwisho, ukimaliza hapo nenda google ingia website inaitwa pipsology nazani kama sijakosea, ukitoka hapo nenda nenda investopedia mule Nako soma kwa mpangilio ukitoka hapo , just andika what is forex Quora then search utalewa machaguo mengi then utapelekwa directly kwenye website ya Quora kuke Sasa utakutana na wataalamu wengi sana Tena wasomi sanaa wahindi,wazungu na nchi zingine utawakuta huko.
Ukimaliza hapo Sasa unaweza lipia darasa la kusoma maana itakuwa ushapata mwanga wa forex madarasa yapo mengi sanaa, utafundishwa strategy ama mbinu za kutabiri soko. Katika kozi kabla ya kusoma hakikisha unamuuliza course content before kulipia contents nzuri kwa uzoefu wangu zinachezaa na haya yafutavyo;
# market structure
#ICT
#BTMM
#SMC, SMART MONEY CONCEPTS
# QUARTERLY THEORY.
# INVALIDATION POINTS OR TURNING POINT.
# LIQUIDITY GRAB
Na mengine mengi wanasoma.
Mtu anayejua forex utampima kwa wingi wa pips anazopata, kwenye mipira wao wanatumia ODDS. the more pipis the more money.
vituo hivi vinahitajika kama unataka kuwa forex trader ama currency speculator.
#elimu ya kutosha
# laptop na smartphones
# bando la kutosha nakudhauri kama uko vizuri apply Vodacom kifurushi Cha superkasi uwe unalipia kwa mwezi tu
# meza na kiti itapendeza kama itakuwa na ofisi kabisa, hakikisha mazingira ni ya utulivu nzuri.
# account ya broker
# account ya bank kwa ajili ya kupokea na kutuma pesa kwa broker nashauri fungua benki ya equity na ABSA vijana wengi wanazitumia sanaa.
Nazani nimemaliza mkuu nakutakia maisha mema,
NB; forex bhanaa unaweza kukukondeshaa vizuri pasipo kuwa na ugonjwa wowote, ni ngumu sana ila ukiimudu umetoboa, narudia Mimi bado sijatoboa napata hela za mboga tu usije kusema mi nguri wa forex
View attachment 2294584