Forex ni kitu cha kweli au udanganyifu tu na kupigwa hela?

Binafsi umeshawahi kukutana na screenshot mtu katoa HATA USD 450? kwa maramoja? Ila naamini umeshawahi ona screenshots kibao zinaonesha USD 5000 kwenye E-wallet hiyo imekaaje
Tumeshatoa mara nyingi sema tu biashara ya forex ina michezo mingi unapaswa kuwa mwelewa sana mwisho ujisimamie.
Kwa Tanzania fuatilia batch iliyoanza forex 2016 walifundishwa watu zaidi ya 2000 mwaka huo kuna mwamba hapa jf anaitwa Ontario tafuta uzi wake .
Leo hii kuna waliofanikiwa na wana majina makubwa na kuna wengi kibao wamefilisika na kuiacha kabisa.
Kwa sasa kama ndio unaanza kuna platform inaitwa moneycashback huwa kuna shindano kila week unafungua demo acvount unawekewa dola 5000 mwisho wa week mwenye profit nyingi wanapewa pesa kuanzia 500$ hili shindano limeanza January mwaka huu linaendelea. Naamini utajifunza kitu huku ukiendelea kujisomea.

Mwisho hakuna sehemu yeyote duniani yenye pesa ya bure tu kwamba unaenda kubeba iwe mziki, mpira, betting.... So forex ni biashara ngumu kama zilivo zingine na ni highly risk business in the world. Nikimaanisha kupoteza 1000$ kwa masaa machache ama dakika 10 ni kawaida pia kupata 1000$ kwa dakika chache ni kawaida
 
Then unaweza kuendelea na hiyo biashara. Kitu cha kunote ni kuwa hiyo 450 usidhani ameitengeneza kwa mtaji wa 200 ujue deposit yake ilikuwa nene na bila shaka ukija kuhesabu withdraws zote alizo fanya hazilingani na mtaji alio weka
Kila mtu anaupeo wake unachofikiri kinaweza kuwa sawa kwako ila kikawa tofauti kwa watu wengine
 
Enzi za ontario? Walio fanikiwa bila shaka ni waandaaji wa semina na waseminishaji na wadau wachache walio trade
 
Mkuu wewe kidogo tunaweza elewana asee
 
Enzi za ontario? Walio fanikiwa bila shaka ni waandaaji wa semina na waseminishaji na wadau wachache walio trade
Mkuu mi nazani wewe hujawahi practice hili game
Tunaomba MT4 Yako tuone, au tueleze kidogo unafahanu Nini kwenye forex.?
 
Ni kama betting unaweza kumuona mtu amepiga kilo mbili ukatamani kuingia mwambie akuoneshe na aliyolost
 
Hio pesa hapo mbona ni nyingi sana? Mimi nikiwa nayo hio wikend lazima unikute visiwa vya comoro ufukweni huko nakula maisha,hotel ya nyota tano 🤣🤣
 
Mkuu wewe kidogo tunaweza elewana asee
kuna watu tulipata pesa za forex ule mwaka mpaka tukatamani kuacha vibarua vyetu mambo baadae yakabadilika kabisa ni mwendo wa kuchoma tu unaweka 100$ wiki moja ya pili una -ve mpaka nikaiacha kabisa. Nikarudi tena kipigo kipigo. Saivi kidogo akili imetulia baada ya kupumzika miaka 3 naweza kupata kitu ila siwezi mshauri mtu aingie akitegemea kuwa tajiri
 
Mambo ni moto mkuu. Pesa ipo ila tambua kuwa 94% ya wanaojaribu hili jambo hawaingizi faida hivyo kuwa na expectation sahihi. Usitegemee mafanikio ya haraka na kamwe usitumie pesa ambayo una njaa nayo.
 
forex ni rahisi kusoma ila ngumu kumaster, has kwa sisi wenye vintaji vidunchu with higher expectations, kwanza jifunze pili tafuta mtaji invest nenda taratibu kuza mtaji huku una master zaid, saiv kuna hizi funding talents pia unaweza jaribu ili ikupe urahisi wa kutrade big money

grow grow thn anza kutafuta pesa itakuchukuwa miaka miwili au mitatu kama upo na resorces zote,
itakuchukuwa miaka mitatu hadi mitano kama resorces ni za kusua sua

ila baada ya apo utakuwa huru kiuchumi na wale waliokuwa wanakuona mwehu ndo watakuelewa wakati uo nawe ndo unawaescape mwisho wanasema trader wanaringa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…