Form Four 2012. Naombeni ushauri wana jukwaa nina result hizi....

Unajieleza vzr sana, unaonyesha umekomaa ki ufahamu japokuwa matokeo siyo. Bado hujashindwa chochote kwa mtizamo wangu jipe moyo hivyohivyo na Mungu akutangulie.
 
ENGLISH na HISTORY sasa bado najiuliza imekuaje. Biology naweza kukubali kutokana na ukosefu wa mwalimu wa somo hilo toka niko form 1. Kitu ambacho kilinifanya kukosa msingi mzuri wa bio.

Sasa inategemea wewe mwenyewe ulikuwa unapenda masomo ya sayansi au biashara au Sanaa.

Ila ushauri wangu ni kwamba inabidi ujifunze masomo yatakayokujenga kuwa mjasirimali kwenye maeneo kama ufundi na kama alivyooanisha mmoja wa wachangiaji hapo juu.
 
Vile vile unaweza kwenda ualimu wa shule ya msingi ukishajipanga kifedha utajiendeleza kwan point hizo zinakidh vigezo vya ualimu lkn kama huupend usiende angalia kwingine usije kufelisisha wadogo zako

Mkuu kwa nafasi ya ualimu kwa sasa wanachukua kuanzia 27
 

computer science! ndio Ndoto yangu kubwa'. lakini sijaua chuo kipi ni kizuri!
 
Pale bungeni kina ndugai na makinda walimtukana sana mbatia. Haya ndo majibu ya nyongeza. Kuna haja ya tume?
 
ENGLISH na HISTORY sasa bado najiuliza imekuaje. Biology naweza kukubali kutokana na ukosefu wa mwalimu wa somo hilo toka niko form 1. Kitu ambacho kilinifanya kukosa msingi mzuri wa bio.

Dogo sababu yako ni nyepesi sana kulinganisha na ugumu wa swali uliloulizwa, kama mpaka hivi sasa ujatambua nafasi yako katika kufanya vizuri kwenye mitihani, na kusingizia kigezo cha mwalimu, basi bado una safari ndefu.

Unakumbuka hii, 25% shule na 75% juhudi binafsi? hii ndio imenifanya leo niwe kazini na mmiliki wa biashara kadhaa mjini hapa, ningetegemea mwalimu kwa asilimia 100 basi naamini ningekuwa miongoni mwa watu wanaoilalamikia serikali kwenye kila kitu.

Jipange dogo kwani, kudondoka na kushindwa kabisa kuamka, ndio maana ya kufeli, nje ya hapo tunaita changamoto tu.
 
Ninatoa shukrani kwa Mungu kwa matokeo nilio yapata.
Wana jukwaa ninaomba ushauri nifanye nini kulingana na matokeo yangu....

Civs-D
Kisw-D
Hist-F
Geo-D
Engl-F
Bio-F
Phy-C
Chem-D
B/Math-D
Div.. IV.28.

Shukrani zangu ziwafikie wote.

Kasome ualimu msingi, AU nenda cerificates kisha diploma, kisha university AU njoo Itende high school, ujiunge form 5 HUKU UKIPIGWA MSASA ku-resit form 4 upate credit 2 zilizo baki, kisha ufanye f.6 then mbele kwa mbele!
 

0.25% shule' 99.75% juhud zang.... Na hapo ndipo nilipo angukia. Sijachoka nimeinuka na safari yangu nataka iendelee hadi nifike nitakapo. Ushauri wenu ndio dira yangu! Namimi ndio nitachagua wapi pakuelekea.
Nashukur kaka
 
Hapo umesema vyema mkuu! Ni bora aenda tuu apige certificate then diploma baadae. Mwisho wa siku na yeye atapiga degree.

ushauri mzuri sana....fanya fasta kwenda kuchukua fom ktk vyuo ya technology kama DIT,MIST na Arusha....ila fahamu kwamba ktk vyuo ivyo vya technology lazima upige short koz inayoitwa pre-entry zen ukifaulu iyo koz ndo unaanza ngazi ya certifiket na diploma...tambua iyo short koz ni ngumu kuliko mtihan wa fom 4 ama fom 6..
 

bora afanye hii kwani chuo sio sawa na form 4 au 6 kwani huko wanakadiliana ila chuo wanajua uelewa wako afanye hivyo kwenda huko dit kuomba nafasi..
 

Acha kuandika pumba, kwanza unajidhalilisha. Utafananisha mitihani ya pre entry au wengine wanaiita bridge course na NECTA? We ujasoma nini? ndio nyie huwa mnashinda vijiweni na kusubiri kuhadithiwa yanayoendelea mashuleni?

Wote waliofeli NECTA wakipiga hiyo short course huwa wanafaulu kwa kishindo, sasa tathmini yako ina ukweli gani?
 
Ninatoa shukrani kwa Mungu kwa matokeo nilio yapata.
Wana jukwaa ninaomba ushauri nifanye nini kulingana na matokeo yangu....

Civs-D
Kisw-D
Hist-F
Geo-D
Engl-F
Bio-F
Phy-C
Chem-D
B/Math-D
Div.. IV.28.

Shukrani zangu ziwafikie wote.

chek nafas ya kuingia chuo pale D.I.T uchukue certifcate kama kwel una ndoto za compter scince..
 
0.25% shule' 99.75% juhud zang.... Na hapo ndipo nilipo angukia. Sijachoka nimeinuka na safari yangu nataka iendelee hadi nifike nitakapo. Ushauri wenu ndio dira yangu! Namimi ndio nitachagua wapi pakuelekea.
Nashukur kaka

Kama juhudi zako zilikua 99.75% basi naweza kusema hii asilimia ujaitendea haki, maana kwa alama ulizozipata, inadhihilisha kuna makosa ulikua unayafanya. Fanya ujifanyie tathmini halafu uyajue makosa yako kwanza, bila ya hivyo sidhani kama utabadili hali. Hizi ni baadhi ya sababu ambazo nadhani baadhi yake ungetakiwa kujibu swali uliloulizwa na mmoja wa wachangiaji.

1)Kwa uzoefu wangu, watu wa namna kama yako wenda mnasoma sana lakini hamuelewi, na hili hamligundui mpaka mnapofeli.

2)Sababu nyingine mnakua mnasoma matango pori, yani mambo ambayo kimsingi hayapo kwenye mtaala, na mnakua heti na mtazamo wa kujiweka tayari zaidi kwa mitihani, kumbe huwa aina ulazima hiyo mitango pori.

3)Pia watu wa namna kama yako huwa hamna mazoea ya kufanya mitihani kwenye vituo mbalimbali kwa lengo la kujifanyia tathmini, huwa mnajiamini kupita kiasi kuwa mko vizuri, mwisho wa siku NECTA inawapakata.

4)Huwa mnasubiri walimu wawaletee kila kitu, wawahamasishe msome na mengine mengi kupitia walimu, hayo ndio matokeo yake.

5)Huwa hamna tamaduni na desturi ya kujadili na wenzenu juu ya mustakabali wenu mnapo kuwa shule, kujadili kuhusu masomo, past papers n.k

6)Huwa hamna ukaribu na wanafunzi wa shule zingine, hapa naongelea mahusiano yako na wanafunzi wa shule nyingine, lakini haswa katika masomo, mnapokuwa na mahusiano mazuri kimasomo na shule zingine, inakupa fursa ya kujua yanayoendelea huko, ambayo kimsingi yanakusaidia katika ufaulu wako.

7)Huwa hampendi kusikiliza maono, ushauri, mwongozo na maelekezo kutoka kwa waliowazidi, wenda kielimu au kiumri, huwa mnamisimamo na mawazo yenu hata kama mawazo hayo sio sahihi.

8)Huwa hamna vipaumbele mnapokuwa shule, hii inawafanya mnafanya mambo mengi kwa wakati mfupi na mwisho wa siku yanatokea haya, wanafunzi wengi mnatamani kujua kila kitu mnapokuwa O-level, sasa usipotenga muda wa kutosha katika kujisomea na kufanya mazoezi mbalimbali, basi lazima hile kwako, huwezi kuendesha elimu huku kulia kwako kuna club, mademu na tungi. Kushoto kwako kuna facebook, twiter,skype, whats up na bbm. Nyuma kuna kazi za nyumbani na changamoto zingine za kifamilia. Mbele kuna NECTA, kazi yake kubwa ni kufanya assessment ya yale yote mliojifunza mnapokuwa shule, kama mmeelewa au lah.

Kati ya hizo sababu nilizo ziorodhesha hapo juu, wewe jiangalie na ujifananishe na kila sababu moja moja hapo, halafu ufikie hitimisho ni kipi haswa kimekufanya uangukie pua.
 
Jiunge na M4C bwana mdogo tena omba kitengo cha kutembeza kapu wakati wa mikutano mbona shavu Hilo mdogo wangu
 
Kasome ualimu msingi, AU nenda cerificates kisha diploma, kisha university AU njoo Itende high school, ujiunge form 5 HUKU UKIPIGWA MSASA ku-resit form 4 upate credit 2 zilizo baki, kisha ufanye f.6 then mbele kwa mbele!

hata ualimu kuna mchujo mkuu mwisho dv iv ya 27, ishu akaanze crtfct ya chochote anachokpenda kulingana na cfa zake kitaaluma.
 
Pale kwenye shule ya mlugo kuna nafasi za kazi ya mlinzi mcheki atakupa shavu kwani kwa matokeo haya kafurahi kupata walinzi wengi
 
bwana Kel.G kama uko kweli una malengo mazuri huu ushauri ni wa mwimu sana....kama mdau alivyosema...na nna amini hivi vyuo ndio chaguo sahihi kwako hasa kwa kozi unayotaka......
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…