Najua kuwa SHADIYA KARUME aka MKEWE RAIS KARUME ameshachukua kwa nguvu open space zote na kawapa wataliii including Nyumba ya mayatima ....Huko Pemba nasikia ndio anaiba kwa mile wala si kwa Acre
Wana JF znz tunaomba input zenu kwenye hili
Zenj kuna tatizo kubwa kuhusu Open spaces na hasa katika Halmashauri ya Manispaa ya Zanzibar.
Halmashauri hii imeundwa na sehemu mbili kubwa, Mji Mkongwe na Ng'ambo. Katika Mji Mkongwe kuna asasi mbili zinazo simamia maendeleo yake, ambazo ni Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe na Halmashauri ya Manispaa.
Katika Mji Mkongwe kuna open kadhaa ambazo ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya Uendelezaji wa mji Mkongwe huku zikipata huduma toka katika Manispaa. Open space hizo ni pamoja na Kelele Square, Jamhuri Gardens, Forodhani Gardens, Mnazi Mmoja Playgrounds na Donge Gardens.
Kelele Square, baada ya Serena Hotel kuingia Zenj walikubaliana na Manispaa kuifanyia matengenezo, na sasa ipo katika hali nzuri na inaendelea kupata huduma toka katika Manispaa na hoteli hiyo. Aidha dhumuni lake la kuwa public open space lipo palepale na sasa inatumiwa zaidi na madereva teski na mapapasi. Umiliki wa eneo hili upo chini ya Mamlaka ya Mji Mkongwe.
Jamhuri Gardens, imeendelea kuwa bustani nzuri kwa wanafunzi wa skuli jirani, aidha ni njia ya mkato wa wakaazi wa Wireless, Kikwajuni na Kisimamajongoo. Mapema mwaka 2000 ilifanyiwa matengenezo ikiwa na kuongezwa kwa mnara wa saa na yule mfadhili maarufu wa Malindi sport club. Umiliki wa eneo hili una utata kidogo kutokana na baadhi ya eneo kuwepo katika eneo la Ng'ambo.
Forodhani Gardens, Ni bustani maarufu na yenye kutumiwa na mamia ya wakaazi katika mji huo. Hii imesababisha kuchakaa kwa haraka sana kwa bustani hiyo. Mashirika na asasi mbalimbali mara kwa mara wamejaribu kuchangia katika kuifufua bustani hii na mafaniko hayakuwa ya uendelevu.
Mojawapo ya asasi hizo ni Zayadesa ambayo iliweza kidogo kufanya matengenezo wakati wakisubiriwa Agha Khan kuja na project yao. Agha Khan walianza kuonyesha hamu ya kuifanyia matengenezo bustani hiyo tokea mwaka 1994. Matengenezo yao ilikuwa ni pamoja kuitanua bustani hiyo kwa mita kadhaa kuingia baharini.
Chini ya Sheria za Mji Mkongwe na Wizara ya Ardhi na Mipango Miji, sio rahisi kwa bustani hiyo kuuzwa. Zaidi ikumbukwe kuwa Agha Khan wamekuwa wakishirikiana kwa muda mrefu na Mamlaka ya Mji Mkongwe katika kuendelea kuifadhi na kuendeleza mji huo ambao sana una hadhi ya
Heritage City