Forojo Ganze (Master), mchawi maarufu aliyeanzisha Mwenge wa Uhuru

Ndio maana hii nchi haiendelei pamoja na kuwa na kila kitu. Nyerere na Ushirikina wake umelicost Taifa sana. Nchi iliyo kabidhiwa kwa mizimu/majini na kwa shetani lazma iwe na viongozi wapuuzi na wa binafsi kama Tanzania. Ila kuna watu wapo field kuiangusha hiyo ngome ya kishirikina na kiahetani inayo ishikilia hii nchi na kuifanya kuwa Masikini na Raia wake kuwa waoga na wajinga.
 
Kunambo mengine ni aheri kutoyajua maana ukiyajua halafu ukayatilia maanani unaweza kushindwa kufanya mambo ya maana..

Jaman umasikin wetu, hautokan na mwenge, ila unatokana na watu wachache kujitajirisha, na kutumia umasikin wetu kujipatia fedha..

Iwe ni kweli au uongo haindoi dhana nzima ya kuleta mshikamano, ila kama ni uongo kunasiku hautakimbia huo mwenge..

Ila pia tuwe tunauliza na vyanzo vya hizi habari, isije kuwa tunaaminishwa uongo na sisi tunauamini
 

sio kweli,Mungu muumba ni mmoja tu,hii mingine ni ya uongo.sio kweli kuwa mataifa yaliyoendelea yameendelea kwa sababu ya kukumbatia Miugu yao.et mfano America,ulaya ba Asia.mfano nchi za ulaya zilikuwa zikiamini katika Miungu mbalimbali wagiriki walikuwa na miungu mingi lakini Zeus ndiye mkuu,warumi pia miungu mingi lkn mkuu Jupiter.uko uarabun Mungu mingu lakin mkuu hubal(Allah).lakin ulaya ya Leo na Amerika ni wakristo wameacha dini zao zao za kishenzi na kuupokea ukristo
 
mwendelezo wa imani za kishirikina unajua alama ya menge kwenye mabango ya magufuli inamaana gani??
siku watz mkifunuliwa yaliyo ulimwengu kiza mtajuta kumchagua huyo mtu,kiufupi tu ni mwendelezo wa yale yale
 
Duh.....
 
Magu akiweza kupiga marufuku sherehe za kukimbiza mwenge na bajeti ilotengwa ikaingia kunako miradi ya kimaendeleo nitampa dole gumba.
wanaoamini kua bila mwenge hakuna mshikamano kaeni mkao wa kula maana soon mirija yenu ya ubadhilifu inakatwa
# against Mwenge# campaign imeshashika kasi
 
 
Ninavyojua mimi wazanaki walikuwa na utaratibu wao kupitia kwa watemi wao kuzima mioto yote usiku wa kuamkia mwaka mpya na siku ya mwaka mpya watu ukusanyika kwa mtemi na moto mpya hupekechwa kwa mtemi. Moto huo ukisha waka ulikuwa unawashwa kwenye magogo makubwa kiasi na kuanza maadamano ya kuwasha moto mpya kila familia ya mzanaki. Na ilikuwa ni marufuku kabisa mtu kutumia moto wake binafsi ambao haukutoka kwa mtemi. Kama ikitokea moto huo ukazimika nyumbani kwako ulikuwa unashauriwa uende kuchukua kwa jirani alie na moto wake. Wazanaki waliamini kuwa likitokea tatizo lolote katika himaya hiyo watatafuta kama kuna mtu alijiwadhia moto wake hivyo kukasirisha mizimu yao.
Kwa mawazo yangu naona kama mwalimu aliamua kuendeleza utamaduni wao huo kwa kutumia vifaa vya kisasa ili kila mtanzania akutane na mwanga huo mpya.
Niliuliza wazee wengi wa kizanaki maana ya mila hiyo wao wanadai ilikuwa mila tu basi, lakini kabla ya kuwasha moto mpya matambiko yalikuwa yanafanyika ili kuubariki mwaka huo na kuleta amani na ushirikiano miongoni mwao. Samahani kwa nitakaowakwaza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…