Sang'udi
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 9,138
- 22,236
Kibwagizo cha mwezi
Nasikitika sana, tena sana, kwa msiba mkubwa uliotokea Moshi, Kilimanjaro, kwa Wakristo waliokuwa wakigombea kukanyaga “mafuta ya upako”. Roho za marehemu ndugu zetu zipumzike kwa amani. Amina.
Lakini pamoja na simanzi hii kubwa, ni fursa ya kukumbushana tena jambo. Mungu anasema nasi, na huwa nasema, Mungu wa ajabu hutukiza mambo haya na yale kushadidia maonyo tunayopeana. Mara kadhaa nimefungua kinywa changu kusema na vile vile kuutumia mkono wangu kuandika kutahadharisha dhidi ya imani yetu ya Kikristo inayoporomokea kwenye KUDANGANYA NA KUDANGANYIKA kwa mwendo kasi ajabu.
Nimewaonya wenye “kuamini haraka na kutumika” kama wachungaji (wa kujitangazia) wanavyoamua (“the gullible and manipulable”). Kwa nini watu tunapeperushwa na mafundisho ya kigeni ovyo hivyo? Tusome tena na tena Ebr 13:7-9. Hivi kukanyaga mafuta ya upako ndiyo kitu gani? Kiroja kama hicho kinakutikana wapi katika Biblia? Kwa nini mtu akija na ubunifu wa uongo namna hiyo, hatumgutukii? Watu wanashobokea uongo kwa maelfu. Aibu kweli kweli! Nasikitika watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa (Hos 4:6).
Je, uongo haujajidhihiri mchana kweupe katika mkasa huu? Mtu anakufaje wakati yupo kwenye kukanyaga kitu chenye baraka? Baraka i wapi kama hapo hapo inaposemwa ipo mtu anadhurika? Na hata baada ya kufa, uwezo wa maombezi na kufufua, tunaotamba kuwa nao, tukishiba maharage na ugali wetu, uko wapi?
Mbona marehemu wanapangiwa mipango ya kuzikwa tu? Wafufuaji wako wapi? Wameingia mitini? TUMEUMBUKA “WAJAMENI!” KWA MAMBO KAMA HAYA TUNAUFEDHESHA SANA UKRISTO!
Nimewasihi, mara kusihi, watu tusidanganyike. Nimewataka, mara kuwataka, waumini tusitikisike na mafundisho ya uongo. Mara nyingi, hata wengine wananiona “domo kaya”, nimetaka Wakristo tuwe imara (tuwe “the unshakable”).
Hivi ya Joseph Kibwetere hayakusema kitu kwetu? Wangapi walikufa tarehe 16.3.2000 kule Uganda? Ule msiba wa Wakristo waliokufa, mwaka jana, kule Zambia, kwa kunywesha JIK, haukutuambia chochote? JAMANI NJAA YA MIUJIZA ITATUUA!
Lakini si kwamba Kristo na Maandiko hayajatuonya. Tatizo letu ni kutoambilika tu. Kwa nini hatusikii “cha mhadhini wala cha mwosha maiti?” biblia imesheheni maonyo. Tumeonywa sana hata sasa sasa hivi rudia kusoma Mt 12:38-40, 24:23-28, Mk 13:21-23, 2Thes 2:9-12 na 2Tim 4:1-5 ukumbushwe tena.
Ndugu zanguni, hii ni hatari, tena hatari kubwa sana.
Hasara kubwa inatunyemelea. Hasara inabisha hodi mlangoni petu. Katika njaa hii, siyo tu tutapoteza uhai huu wa kibailojia, bali pia hata ule uzima wa milele. Kifupi, tujiandaeni kwa kifo cha pili (Ufu 2:11). Ole wetu!
Lakini kwa kuwa tunapuuzana tunapoonyana, tusubiri ya Firauni sasa. Yaliyotokea ni ya Musa tu, ya Firauni yaja. Na kwa kuwa Kanisa Katoliki nasi tumepatwa na ugonjwa wa KUIGA KIUPOFU, ninajua ya Firauni yatotokea kanisani mwetu pia.
Miaka michache kidogo iliyopita Wakatoliki tungeliweza kusimama pembeni na kusema matukio ya aibu namna hiyo si yetu. Lakini sasa hivi na sisi tupo katika foleni ile ile na tunaelekea kule kule kwa sababu tumetumbukizwa katika UIGAJI WA KIUPOFU.
Lakini yatakapotokea hayo kanisani mwetu, mimi sijui tutaficha wapi sura zetu! Lakini nadhani ingekuwa afadhali yakitokea baada ya mimi kuitaliki dunia hii.
Mzee wenu Padre Titus Amigu.