Awe mpole..
Alifungwa kwa hujuma za kijinga .
Brave one, heshima mbele,
Naomba udadavue kidogo habari hii hasa kuhusu ni mahakama hipi imepitia hiyo hukumu au hiyo rufaa, na ilikaa lini chini ya nani na maamuzi hayo yametolewa lini na chombo hicho tajwa? Haki upatikana na kutamwa na mahakama na si kupitia kwa "promota". Hivyo basi nachelea kusema habari hii ni tetesi na inatakiwa ibaki kama tetesi mbaka hapo itakapothibitishwa.
Jera sitaki hata pasikia.
Ngoja niendele kuwa Law Abiding Citizen
Yule askari polisi aliyekula njama na hakimu wakampiga mvua sijui watakuwa wanajiskiaje. Anyway, kushinda kwa rufaa ni ishara kuwa adhabu haikuwa proportional na kosa. Wataalam wajifunze kutenda kazi kwa kutumia utaalam wao na sio mihemko au visasi.
nenda kaulize pesa waliyotoa kuachiwabondia nyota zaidi nchini, francis cheka ameachiwa huru.
cheka ameachiwa huru baada ya kushinda rufaa yake aliyokata kupinga kifungo cha miaka mitatu gerezani.
tayari cheka alianza kutumikia kifungo hicho mjini morogoro. lakini taarifa za uhakika zinasema ameachiwa leo baada ya kushinda rufaa hiyo.
tayari ameachiwa, lakini tunashughulikia masuala kadhaa kumalizia ishu hiyo. Ila tayari yuko nje, alisema kaike siraju, promota wa ngumi za kulipwa aliyekuwa akipambana kuhakikisha cheka anatoka.
cheka alihukumiwa kwenda jela baada ya kumtwanga na kumuumiza meneja wa baa yake mjini morogoro akimtuhumu kumsababishia hasara.
chanzo: salehjembe blog
Sasa Ndiyo Atakuja Kuwapigeni Ngumi Hadi Nyie Wenyewe MTAKIMBILIA Gerezani Humo Kujificha. Pole Sana Francis Cheka Na Taarifa Hii Nimeipenda Kwani Wewe Ndiyo Lenox Lewis Wa Tanzania ILA Tu Sasa Tulia, Jirekebishe Na Acha Hiyo Kampani Yako Ya Wavuta Bangi Hao Akina........,..........,........! Mshukuru Mwenyezi Mungu, Tulizana Akili, Jipange Upya Na Tunataka Utulipe Fadhila Kwa Kufanya Vizuri Ktk Ndondi Na Nina Imani Kubwa Mno Na Wewe Kwani UNA KILA SIFA YA KUITWA BONDIA Na MPAMBANAJI. Nimefurahi Sana Kupata Taarifa Hii Na Pongezi Pia Kwa Watu Wote Mliopigania Hadi Kuhakikisha Kuwa Francis Cheka Leo Anakula Chakula Cha Mkewe Na Atapata Hadi Fursa Ya Kuiona MBUNYE Kwa Siku Ya Leo.