Francis Cheka aachiwa huru

Francis Cheka aachiwa huru

kumbe ukifungwa bado unao uwezo wa kukata rufaa??
na je, ukiwa ndani nani hasa atakua anakisaidia kukata?

kuna mawakili (advocates) wanaeza kufanya iyo kazi.
 
Awe mpole..

Sasa Ndiyo Atakuja Kuwapigeni Ngumi Hadi Nyie Wenyewe MTAKIMBILIA Gerezani Humo Kujificha. Pole Sana Francis Cheka Na Taarifa Hii Nimeipenda Kwani Wewe Ndiyo Lenox Lewis Wa Tanzania ILA Tu Sasa Tulia, Jirekebishe Na Acha Hiyo Kampani Yako Ya Wavuta Bangi Hao Akina........,..........,........! Mshukuru Mwenyezi Mungu, Tulizana Akili, Jipange Upya Na Tunataka Utulipe Fadhila Kwa Kufanya Vizuri Ktk Ndondi Na Nina Imani Kubwa Mno Na Wewe Kwani UNA KILA SIFA YA KUITWA BONDIA Na MPAMBANAJI. Nimefurahi Sana Kupata Taarifa Hii Na Pongezi Pia Kwa Watu Wote Mliopigania Hadi Kuhakikisha Kuwa Francis Cheka Leo Anakula Chakula Cha Mkewe Na Atapata Hadi Fursa Ya Kuiona MBUNYE Kwa Siku Ya Leo.
 
Brave one, heshima mbele,

Naomba udadavue kidogo habari hii hasa kuhusu ni mahakama hipi imepitia hiyo hukumu au hiyo rufaa, na ilikaa lini chini ya nani na maamuzi hayo yametolewa lini na chombo hicho tajwa? Haki upatikana na kutamwa na mahakama na si kupitia kwa "promota". Hivyo basi nachelea kusema habari hii ni tetesi na inatakiwa ibaki kama tetesi mbaka hapo itakapothibitishwa.
 
Maskini bar manager!!ndo keshakosa haki hivyo,na ndiyo tabia ya pesa,hubadilisha ukweli kuwa uongo&vise versa,sasa mshtaki tu kwa Mungu maana yale makonde aliyokusukumia siku ile ni madogo,amejipanga kukuporomoshea mazito zaidi akifika mtaani!! Get ready.
 
Alifungwa kwa hujuma za kijinga .

Tena Ni Za Kisiasa Zaidi Kwakuwa Francis Cheka Anakubalika Zaidi Hapo Town Na Akawa Anataka Kuhamia Kwa ( Wana UMOJA Wetu Wa Kiupinzani ) Hivyo Nia Yake Ilikuwa Ni Kumshtaki Tu ILI Akisema Agombee Ubunge Kipengele Cha Kuwahi Kushtakiwa Na Kuwekwa Gerezani Kimmalize Na Kwa Sasa Hawezi Tena Kugombea Huo Ubunge Kwani Imeshakula Kwake, Na Ni Huyo Huyo Tena Bondia Francis Cheka Alikataa Kufanywa Nae Kuwa Begi La Kusafirishia Sembe Mwaka Jana Na Mhusika Mwenyewe ANATUBEBA Sana Na Mno Safarini Morogoro, Moshi - Arusha, Hadi Songea Sasa Na Leo Kaanza Kujumuika Na Wenzake Ktk Kutupangia Bajeti Ya Mapato Na Matumizi Kwa 2015/2016. Huwa Hana Mpinzani Ruti Ya Msamvu Na Ubungo Terminal! Kazi Kwenu.
 
Brave one, heshima mbele,
Naomba udadavue kidogo habari hii hasa kuhusu ni mahakama hipi imepitia hiyo hukumu au hiyo rufaa, na ilikaa lini chini ya nani na maamuzi hayo yametolewa lini na chombo hicho tajwa? Haki upatikana na kutamwa na mahakama na si kupitia kwa "promota". Hivyo basi nachelea kusema habari hii ni tetesi na inatakiwa ibaki kama tetesi mbaka hapo itakapothibitishwa.

Global nao wanakuja na hii story:
BONDIA Francis Cheka aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwenda jela kwa kosa la kumpiga ngumi meneja wa baa yake, amebadilishiwa adhabu ya kifungo. Cheka amechiwa na kutoka gerezani na sasa anatakiwa kutumikia kifungo cha nje.
 
Jera sitaki hata pasikia.
Ngoja niendele kuwa Law Abiding Citizen

Mkuu mwombe MUNGU tu akuepushie haya makitu hayatabiriki, wengi huwa wanapelekwa huko kwa kusingiziwa. Hivyo hata ukitii sheria kuna siku unaweza kujikuta umo ndani ya house na usipoangalia jamaa wanakupipe!! Sijui kama Cheka hii kiti ameiepa!
 
Acha kudanganya watu. ametolewa kifungo cha gerezani na kupewa kifungo cha nje yaani afanye kazi za jamii.hajakata rufaa yoyote.ni taratibu za kimahakama baada ya kufanya mapitio ya hukumu.
 
Yule askari polisi aliyekula njama na hakimu wakampiga mvua sijui watakuwa wanajiskiaje. Anyway, kushinda kwa rufaa ni ishara kuwa adhabu haikuwa proportional na kosa. Wataalam wajifunze kutenda kazi kwa kutumia utaalam wao na sio mihemko au visasi.

Kumbe kulikua na njama?
 
huyo naona wabaya wake walimtengenezea ishu asiendelee kuwatwanga
 
Mkuu Amavubi nauliza tuu, bado hujapata updates ya hii habari yako maana kuna maswali aliuliza Mkuu Shadow @11:03 nadhani yanahitaji majibu.
 
Mkuu Amavubi nauliza tuu, bado hujapata updates ya hii habari yako maana kuna maswali aliuliza Mkuu Shadow @11:03 nadhani yanahitaji majibu.
mkuu lwo hakukua na umeme ndio naingia net tena
 
[h=3]BONDIA FRANCIS CHEKA SASA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA NJE[/h]

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mororogoro leo imetengua adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela kwa Bondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka na badala yake atatumikia kifungo cha nje na kulipa fidia ya Shilingi milioni moja.

Cheka alikuwa akikabiliwa na kosa la kumpiga na kumjeruhi Bahati Kibanda, ambaye alikuwa ni meneja wa baa yake iitwayo Vijana Social Hall iliopo mjini Morogoro.

Cheka anatumikia kifungo chake cha nje kwa kufanya kazi za serikali kwa muda wa masaa manne kila siku kwa kipindi chote cha kifungo hicho.

Bondia maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka akipatiwa maelekezo kutoka kwa askari.Picha na Maktaba.

source Issa Michuzi
 
cheka2%2btua.jpg

bondia nyota zaidi nchini, francis cheka ameachiwa huru.
cheka ameachiwa huru baada ya kushinda rufaa yake aliyokata kupinga kifungo cha miaka mitatu gerezani.

tayari cheka alianza kutumikia kifungo hicho mjini morogoro. lakini taarifa za uhakika zinasema ameachiwa leo baada ya kushinda rufaa hiyo.

“tayari ameachiwa, lakini tunashughulikia masuala kadhaa kumalizia ishu hiyo. Ila tayari yuko nje,” alisema kaike siraju, promota wa ngumi za kulipwa aliyekuwa akipambana kuhakikisha cheka anatoka.

cheka alihukumiwa kwenda jela baada ya kumtwanga na kumuumiza meneja wa baa yake mjini morogoro akimtuhumu kumsababishia hasara.

chanzo: salehjembe blog

nenda kaulize pesa waliyotoa kuachiwa

cc jaji mkuu

awe na adabu mtaani asidharau watu kwa akili zake za ngumi
 
Sasa Ndiyo Atakuja Kuwapigeni Ngumi Hadi Nyie Wenyewe MTAKIMBILIA Gerezani Humo Kujificha. Pole Sana Francis Cheka Na Taarifa Hii Nimeipenda Kwani Wewe Ndiyo Lenox Lewis Wa Tanzania ILA Tu Sasa Tulia, Jirekebishe Na Acha Hiyo Kampani Yako Ya Wavuta Bangi Hao Akina........,..........,........! Mshukuru Mwenyezi Mungu, Tulizana Akili, Jipange Upya Na Tunataka Utulipe Fadhila Kwa Kufanya Vizuri Ktk Ndondi Na Nina Imani Kubwa Mno Na Wewe Kwani UNA KILA SIFA YA KUITWA BONDIA Na MPAMBANAJI. Nimefurahi Sana Kupata Taarifa Hii Na Pongezi Pia Kwa Watu Wote Mliopigania Hadi Kuhakikisha Kuwa Francis Cheka Leo Anakula Chakula Cha Mkewe Na Atapata Hadi Fursa Ya Kuiona MBUNYE Kwa Siku Ya Leo.

Acha utoto wako wa kuchanganya herufi kubwa na ndogo wewe jitambue
 
Back
Top Bottom