GE2025 Francis Forodhan: Uchaguzi Zanzibar ulikuwa wa Huru na Haki

GE2025 Francis Forodhan: Uchaguzi Zanzibar ulikuwa wa Huru na Haki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mkuu wa Idara ya Tathmini na Ufuatiliaji wa Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation ya Francis Forodhan wakiwa ni waangalizi wa ndani wa uchaguzi ameeleza namna Mchakato na uendeshwaji wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar ulivyofanyika katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mkoa wa Kusini Unguja katika Wilaya zote

Ameeleza kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ilifanya maandalizi mazuri ambapo vituo vyote vya kupigia kura vilifunguliwa kwa wakati na hali ya usalama ukiwa umeimarika hukiu wananchi wengi walijitokeza kwa wingi kupiga kura

Aidha ameeleza kama waangalizi wa ndani wanaona uchaguzi ulikuwa wa huru na haki kwani hakukuwa na vitendo vya hujuma kwa wagombea wala wananchi kunyimwa fursa ya kuchagua viongozi wao, pia hakukuwa na viashiria vyovyote vya rushwa, uchochezi wala uvunjifu wa amani katika kipindi chote cha kupiga kura



​
 
Back
Top Bottom