Francis Kahata aaga Simba SC

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Ni baada ya uongozi kumjulisha kwamba hautamuongezea mkataba wake unaoisha mwishoni wa msimu huu.

Kahata amewashukuru wanachama, viongozi na mashabiki wa Simba SC kwa kukaa nae kwa upendo muda wote alioitumikia timu.

Pia anaondoka kifua mbele kwa kuiwezesha Simba SC kutwaa mataji ya ligi kuu Tanzania Bara, na kuiwezesha Simba kutinga hatua ya robo fainali klabu bingwa Afrika mara mbili.

Nimtakie maisha mema na mafanikio tele huko aendako, akumbuke Simba ni nyumbani anakaribishwa muda wowowte atakaojisikia kuitembelea.

UPDATE.

Perfect Chikwende raia wa Zimbabwe nae kuna uwezekano mkubwa akaachwa kutokana na kiwango alichokionesha toka asajiliwe na Simba SC kutomridhisha kocha.
 
Simba washaua kipaji kingine huku

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Bora alivyoondoka, sijawahi kumkubali huyo jamaa. Ana ball control nzuri lakin hana threat kiivyo anapofikia final third, mpira wake ni wa show off. Halaf nikusahihishe hapo juu umesema kaisaidia Simba kufika robo fainali mara mbili sio kweli, wakat tunaingia robo mwaka juzi hakuwepo. Msimu uliopita kachangia kwa kiasi kikubwa kutolewa na UD Songo kwasabab hakuwa na madhara kule mbele.
Naupongeza uongoz wa Simba kwa kuachana na huyo mtu hakuwa na mchango mkubwa tunaouhitaji kutoka kwa foreign player. Ukiona mchezaji anaachwa na Simba ujue garasa ilo.
 
Hakukuwa na haja ya kumleta perfect wakati tulikuwa na kachi.

Kila la kheri kwake
 
Kahata ana miaka mingapi Simba?
 
Nampongeza kwa mchango wake uwanjani na nidhamu ya hali ya juu sana ndani na nje ya uwanja alioionyesha kipindi chote alichokuwa Simba. Kila la heri mguu "kijiko". Kwa "level"ilipofika Simba sasa hivi kulikuwa hamna namna ya Kahata kuendelea kuwepo pale Simba kutokana na kiwango chake. Kahata ni mchezaji mwenye kiwango kizuri lakini tukatae tukubali kwa sasa Simba inakwenda hatua nyingine zaidi kwani sasa hivi wanaanza kuwafuata huko juu vigogo wa Afrika walipo. Kwa njaa ya mafanikio zaidi ninayoiona kwa Mo na bodi ya Simba nategemea kutakuwa na mshtuko kwenye usajili wa Simba mwaka huu. Kwa mtizamo wangu wakati watu wanashangaa Kahata kuachwa kwenye usajili mimi naona kuna wachezaji wengine wawili/watatu wa kigeni tena wakutegemewa kabisa wataachwa kwenye huu usajili unaokuja. Na wataachwa si kwasababu ya viwango vyao vimeshuka hapana bali Simba sasa hivi inahitaji wachezaji wawili mpaka watatu wa kigeni wenye viwango kuwazidi hao watakaoachwa ili iweze kundelea zaidi ya robo fainali ya CL ilipogotea mara mbili.

Narudia tena kila heri uendako mwamba Kahata umeutendea haki mkataba wako na Simba. Kiwango chako hakijashuka ila ni wakati tu ndio unaenda mbio kwani kwa sasa Simba inahitaji mtu/watu wenye uwezo zaidi yako ili kuimalizia safari yao ya mafanikio Afrika.
 
Perfect, kagere na wawa usishangae wakaachwa japo ni wazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…