Franco Mtui apooza mwili mzima

Franco Mtui apooza mwili mzima

Dedicated to the hommies that we've lost....

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=VdX31hyh6HM]YouTube - R Kelly - To All The Homies We Lost (i wish remix)[/ame]
 
Oloronyo, sikujui hunijui lakini huna ubinaadamu kabisaaaa, the guy is a vegitable now wewe unatuhabarisha about his past, zitatusaidia nini na yeye zinamsaidia vipi? Usimtukane Mamba ilihali hujavuka mto kaka.

...duu, temea chini bana,...Frank kapata paralysis kama itakuwa permanent au kwa muda tunamuachia Mw'Mungu na madakitari wake, hiyo vegetative state au 'vegitable' uliosema sio kabisa ya kumuombea mkuu...
 
Franco aliyewahi kumiliki Bar ya kwanza ya aina yake ya kukesha usiku ya AQUA pale Msasani na pia Video library ya Aqua pamoja na watoto wa Kida WOS umesahau kuhusu UFI?

La UFI + Kida.... tusimuingize Franco kwa maana hata wewe watu unaojikuta nao katika shughuli zako sidhani unaanza kuuliza CV/Resume na geneology....
Tumwombee speedy recovery tu huyu mwenzetu.
 
kama alivyosema mzee Muyaka:

Mbona umeghafilika kwa jambo lisilo na shaka?

Shetani umemshika na kumuacha Nabia?
 
Lalasheee! Habari za kusikitisha nimezisoma kwa yule Nanhii wa Tegeta kuwa yule Will Smith wa wetu enzi zile 1990-2000 Bw.Franco Mtui amepooza mwili wake mzima alipopata ajali ya "kuangukia shimoni shambani kwake" na kwa sasa amelazwa hospitali ya Netcare Rehabilitation Centre J'burg.
Francis Mtui aka Franco alikuwa kijana mtanashati na pia sana enzi hizo za miaka ya mwisho ya mzee Ruksa ambapo wakati huo alikuwa anauza magari,alifunga pingu za maisha na Perece Kirigiti mwishoni mwa miaka ya 90 ambapo ilifuatiwa na reception ya kukata na mundu kama sio shoka iliyofanyika katika viwanja vya pale ilipo Multichoice Dar,ndoa yao iliyojaliwa kupata mtoto mmoja,iliingia doa na wawili hao walitengana mwanzoni wa miaka ya 2000 na hiyo kupelekea Franco aliyewahi kumiliki Bar ya kwanza ya aina yake ya kukesha usiku ya AQUA pale Msasani na pia Video library ya Aqua pamoja na watoto wa Kida,kuwa mlevi mbwa,na hivyo kumfanya awe anakunywa mpaka pombe za kienyeji nk
Mara kwa mara alikuwa anaokotwa amelala pembeni ya barabara na siku za karibuni alipotea katika hadhara hadi Mkuu wa nanhii alipomuweka katika Blog yake,kwa kuwa kule kwa mkuu wa wilaya ya nanhii anabania maoni,nikaona nilete habari hapa.
Wito wangu kwa hawa Macelebs wetu wa bongo wawe makini katika maisha haya ya sasa wakati huo wakumbuke sana baadaye kwani mambo yanaweza kuwaharibikia. Hospitali hiyo pia amelazwa Mzee wetu Timoty Apiyo na Mwandishi Athumani Hamisi.
Tunamtakia kila la heri Bw.Francis Franco Mtui apone haraka na amkumbuke muumba wake.

Hii ni kejeli. Je unahuzunika kwa ugonjwa wake au unafurahia?? Yaelekea unafurahia moyoni kwa kuwa either ulikuwa na bifu naye?? Alikuchukulia nanihiii nini?? Msamehe bure.
 
Huyu Franco..ni yule alikuwa anakaa o'bay miaka ya 80s (mweupi hivi) na alikuwa anapenda sana kucheza "break-dance" miaka ile?
POLE SANA Franco.
 
Erooo,Habari hii ningeandika hivi; Habari za kusikitisha nimezisoma kwa yule Nanhii wa Tegeta kuwa yule Will Smith wa wetu enzi zile 1990-2000 Bw.Franco Mtui amepooza mwili wake mzima alipopata ajali ya "kuangukia shimoni shambani kwake" na kwa sasa amelazwa hospitali ya Netcare Rehabilitation Centre J'burg.

Wengi hapa wangeuliza; Ni nani? etc

Wana JF kama mbwayi mbwayi tu.
Mbona David Mac Mosha aliyeuawa na mbwa kule Kawe Beach hamkumvamia aliyeleta mtundiko ule hapa?!

 
Hii ni kejeli. Je unahuzunika kwa ugonjwa wake au unafurahia?? Yaelekea unafurahia moyoni kwa kuwa either ulikuwa na bifu naye?? Alikuchukulia nanihiii nini?? Msamehe bure.

Mkuu umemwuliza huyu jamaa maswali ya msingi sana,hii thread imekaa kibifu bifu yaani ni kama vile huyu jamaa alikua na ugomvi na huyu anaeumwa,kwa hiyo inavyoonekana na kwamba anafurahia sana.Tujaribu kumwelewesha hii tabia si nzuri kushangilia wenzetu wanapofikwa na matatizo kama haya.
 
sasa Morani, utawala wa Mzee Kida kiwanda cha UFI na ajali ya Franco Mtui inahusiana vipi bana? ...

Ahsante sana Mbu, hakuna uhusiano wowote wa ajali ya Franco na akina Kida au hata utawala wa Kida alipokuwa UFI.
 
Imekaa kama kaumbea umbeya fulani hivi! Inatuhusu nini sisi hii?

Well, inahusu jamii nzima. Yeyote anae pozi kupiga picha kupeleka MICHUZI huyo hataki privacy, anatamani kujadiliwa na jamii, ugonjwa wake, maisha yake, ya nyuma, ya mbele, familia, umbea wake, sura yake, biashara zake... Ana enjoy himself. Picha ikitoka MICHUZI inaenda JF, halafu Dar-Hotwire, then UTAMU. Yeye anafurahia.

4898d1245230582-franco-mtui-apooza-mwili-mzima-franco.jpg
 
4898d1245230582-franco-mtui-apooza-mwili-mzima-franco.jpg

naam itabidi nirudi tena kwa bwana Muyaka ambaye anasema ....

UNAJIFANYA MTESI
KWA MOLA WAKO MKWASI
UNAVITUPA VIASI
SINA LA KUKUAMBIA
 
Back
Top Bottom