Frank de Boer kocha mbovu anayeng'ang'ania kufundisha soka

Frank de Boer kocha mbovu anayeng'ang'ania kufundisha soka

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Huyu ni kati ya wachezaji wakongwe waliofanya vizuri lakini wasioweza kufundisha soka , cha ajabu anang'ang'ania jambo asiloliweza.

Alitimuliwa Ajax na InterMilan kwa kiwango kibovu kabisa kwenye timu hizo ( Shukrani kwa viongozi wa timu husika kwa kuona mbali ).

Kama haitoshi leo akiwa Kocha wa timu ngumu ya Crystal Palace ameleta gundu baya sana kwa timu hiyo kuchakazwa bao 0 - 3 na timu ngeni iliyopanda daraja ya Huddersfield Town .

Namtabiria kutimuliwa haraka sana .

..... Up dates ............

De Boer sacked after his first four Premier League all ended in defeat

Crystal Palace became the first in Premier League history to loose their opening four fixtures without scoring a goal .

His three years deal Terminated after 77 days only .

Roy Hodgson , the Former England Manager may take charge
 
jana nimeshangaa sana kwa crystal kupigwa tatu... kumbe de boer ni kirusi ndio sababu
Huyu jamaa ni kocha mbovu ambaye hata sijui anapewaje kazi ! Ameiharibu Ajax mpaka sasa bado inapepesuka .
 
Huyu jamaa ni kocha mbovu ambaye hata sijui anapewaje kazi ! Ameiharibu Ajax mpaka sasa bado inapepesuka .
de boer kubeba ligi ya uholanzi mara 4 mfululizo, kabla ya hapo ajax walikua hawajaguza ubingwa wa ligi tangu 2003. na inter milan tim lao ni bovu huwezi kumlaumu de boer. hata mancini na ranieri walionekana sio wazuri walivokua inter ila wamebeba ubingwa wa epl...hio tim wanafukuza kocha kila mwaka hata sasa hivi wana kocha mzuri sana ambae amefanya vizuri roma msimu uliopita ila inter watamfukuza tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ligi ya uholanzi si kipimo halisi , angalia kocha wa celtic anavyofanya , akitoka nje tu mdebwedo ! De boer hana uwezo wa kufundisha nje ya uholanzi , hata hivyo msimu wa mwisho alivurunda vibaya mno !

Ni sawa useme Steve Maclaren ni kocha .
 
Hivi huyu kocha bado hajatimuliwa tu ?
katimuliwa, ila hapo ajax umemsingizia, amefanya vibaya crystal palace na inter ila ajax amefanya maajabu, walishapotea ajax yeye kawabebesha makombe manne mfululizo, ameeka rekodi yake uholanzi. hilo la uholanzi kutokuwa ligi bora ni jengine.

na si kweli kwamba eti amefukuzwa ajax, hakufukuzwa bali alishika nafasi ya pili akajiuzulu, kocha ambaye amebeba kombe mara 4 mfululizo ligi ya uholanzi, ni rekodi yake pekee, halafu akashika nafasi ya pili akajiuzulu sio mtu wa kawaida kumsema eti hajui kufundisha.

na hata kama umeangalia mechi ya crystal palace ya jana wametawala mpira, wamepiga mashuti 23, bahati tu haikuwa yao,
 
Back
Top Bottom