Frank Lampard ateuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya Everton

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari,

Frank Lampard ametuliwa kuwa kocha wa Club ya Everton na kuchukua mikoba ya Rafael Benitez ambaye amefukuza hivi karibuni.

Frank Lampard ambaye amewahi kuwa kocha wa Club ya Chelsea amepewa majukumu hayo ili kufufua matumaini tena klabuni hapo.

Aliwahi kuwa mchezaji wa Chelsea na sasa ndio kocha mkuu, Frank Lampard amepewa mkataba wa miaka miwili na nusu kurithi nafasi ya Rafael Benitez ambaye alifukuzwa ndani ya mwezi huu, January baada ya kupoteza mchezo wao 2-1 dhidi ya Norwich City.

Everton walikuwa wameshinda mchezo tu katika michezo 13 ya Ligi Kuu ya Uingereza. Hadi sasa Everton inashika nafasi ya kumi na sita kwenye msimamo wa ligi ikiwa na points 19 baada ya kucheza michezo 20.

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu
 
Sidhani kama atamaliza hiyo miaka miwili na nusu ya huo mkataba wake. Maana atasajili vitoto vidogo kwa mkopo kutoka Chelsea! na mwisho wa siku timu itashindwa kuhimili mikiki mikiki ya ligi.
 
Lampard na jinsi Everton ilivyo sidhani kama muda kama huu mwakani bado atakuwa Everton
 
Benetezi ana bahati mbaya sana toka alipoondokaga Liverpool, na mambo kwake hayajakaa vizuri, ila lampard kwa Everton naona anapewa kazi kubwa
 
Sidhani kama atamaliza hiyo miaka miwili na nusu ya huo mkataba wake. Maana atasajili vitoto vidogo kwa mkopo kutoka Chelsea! na mwisho wa siku timu itashindwa kuhimili mikiki mikiki ya ligi.
Ingizi Jipya Wameingia Pamoja Pale Everton Dirisha Hili Dogo

*Dele Alli, Van De Beek & El-Ghazi tukumbuke pia Everton wanakikosi kizuri ambacho kinaweza kuleta ushindani kama misimu mwingine anavyofanya.

Lampard anaamini katika makinda angalia vizuri alivyokuwa Chelsea alivyowaamini watoto wa kiingereza Tammy & Mount Ila Hadi Sasa pale Chelsea mtoto Mount ni cream nzuri sana pale na mchango wake unaonekana.

Tammy pia anatumiwa na Morinho Roma kule na kiwango chake kinaonekana.

Naamini ataleta ushindani na anaweza kudumu na Everton kwa kipindi kirefu.
 
Frankiee si kocha, yule alisabisha Chelsea iwe pahali pabaya
Everton ni timu daraja la kati pale hakuna pressure kubwa sana hivyo basi naona future is bright kwa Everton na Lampard mwenyewe.
 
Ameanza Kwa Ushindi Mnono Kwa Mabao Manne Kwa Moja Dhidi Ya Brentford Kombe La FA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…