Frank Olson: Afisa wa CIA aliyekufa baada ya kuonjeshwa sumu yake Mwenyewe

Frank Olson: Afisa wa CIA aliyekufa baada ya kuonjeshwa sumu yake Mwenyewe

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
7,894
Reaction score
22,679
Wakati vita baridi ikianza kupamba moto miaka ile ya 1950s na 1960s, shirika la kijasusi la CIA lilianzisha program kadhaa zilizohusisha utengenezaji wa silaha za kibayolojia au tuseme silaha za sumu. Silaha hizi za sumu zilijumuisha utengenezaji na utumiaji wa kemikali za kudhibiti akili za mateka wa kijeshi au majasusi wanaokamatwa .

Dawa au kemikali hizi za kudhibiti akili zilijumuisha kutumia dawa za kulevya au sindano za sumu ili kuondoa utashi wa mtu ili atende au asitende jambo pasipo utashi wake. Au pia kumpa kemikali ambayo anaweza kuongea ukweli wote pasipo yeye kujua ameongea ukweli wake kuhusu jambo fulani.

Nataka niwape mfano rahisi. Kwa mfano Maeneo ya bar unakuta mwanaume anamnywesha mwanamke pombe hadi analewa tilalila kisha huyo mwanamke anapelekwa chumbani pasipo utashi au akili yake timamu na kwenda kufanyiwa ya kufanyiwa. Hapo unakuwa umemfanyia mind control au kudhibiti akili yake asijitambue. Au unakuta mtu anapewa pombe au aina fulani za madawa ya kulevya(truth serum) kisha anaanza kuongea ukweli wake wote kuhusu jambo fulani.

Sasa aina hii ya mifano niliyokupa ,wao CIA walianzia kuifanyia majaribio maabara.
CIA walianzisha project au mradi walioupa jina la PROJECT ARTICHOKE au MK- Ultra ambapo mradi huu ulihusiana na kutengeneza dawa au kemikali ambazo ni sumu kwa ajili ya kudhibiti akili za watu yaani mind control tools lengo kuu likiwa ni kumfanya mtu au "subject"atende au asitende wanalotaka kwa kuishika na kuiteka akili yake kwa kutumia madawa.
Mradi huu ulihusisha utumiaji wa kemikali hatari zaidi duniani iliyopigwa marufuku iliyoitwa LSD au Lysergic acid Diethylamide ambayo humfanya mtu kuona maruweruwe(hallucinations )na kuigeuza akili yake kabisa.

Sasa basi Mradi huu wa siri wa CIA ulikuwa ukifanyika kwenye maabara za kambi ya kijeshi ya fort Detrick iliyoko huko Maryland marekani na ikisimamiwa na kitengo cha Special Operations Division (SoD).
Tukija kwenye mada sasa , ni kwamba kitengo hiki cha SOD hapo fort Detrick aliyekuwa mmoja wa mastermind akifanya kazi hii alikuwa daktari na mtafiti mmoja aliyeajiriwa na CIA aliyeitwa Frank Olson ambaye kitaaluma alikuwa ni mbobevu kwenye uundaji na utengenezaji wa silaha za sumu za kibayolojia akishirikiana na baadhi ya madaktari wa ujerumani waliotoroshwa na marekani kule ujerumani kwa siri baada ya vita kuu ya pili ya dunia kwenye operesheni iliyojulikana kama operation paperclip.
Huyu bwana alikuwa akifanya kazi chini ya SOD akiwa na wenzake kuanzia mwaka 1951.
Frank_Olsen_(1910-1953).jpg

Frank olson daktari na mwanabayolojia ambaye alikuwa mtaalamu aliyeajiriwa na CIA katika utafiti na matumizi ya kemikali za sumu za kufanya mindi control.

Sasa siku moja November mwaka 1953, huyu bwana Frank Olson akiwa na maafisa wenzake akiwemo mkuu wa kitengo hiki cha SOD aliyeitwa Vicent ruwet na wengine watano walialikwa kwenye sherehe kwenye safe house moja ya Siri ya CIA iliyoko Maeneo ya deep creek lake huko Maryland nchini marekani. Kwenye sherehe hii pia alikwepo mkurugenzi wa kitengo kingine cha CIA ambacho kilijulikana kama CIA"s Technical service Staff aliyeitwa Sidney Gottlieb pampja na naibu wake Robert lashbrook.
gottlieb-a.jpg

Huyu ni Gottlieb ambaye alikuwa ni mastermind mmojawapo wa hii project ya CIA.


Mbali na sherehe hii kulikuwa na ajenda zilizojadiliwa kuhusu matumizi ya kemikali za sumu zilizokusanywa sehemu mbalimbali duniani na pia matokeo yake pale zinapotumiwa na "subject".
Sasa basi katika party hii kulifanyika jambo hatari sana tena kwa siri kubwa mno. Waliamua kufanyia majaribio hapohapo kwenye party.
Huyu naibu mkurugenzi wa TSS bwana Robert lashbrook aliamua kuchanganya kwa siri sana dozi milligram kadhaa za LSD kwenye chupa ya pombe kali ya whisky aina ya Cointreau. Lengo lake ni kutaka kupata jibu mojawapo katika maswali kadhaa ya madhara ya matumizi ya LSD.Kati ya maafisa wa SOD waliohudhuria ni wawili tu hawakunywa pombe hiyo ila Olson na wenzake walikunywa. Reaction ilipoanza kujitokeza baada ya kunywa kinywaji hiki ilionekana side effects zilimuathiri sana Huyu Frank Olson. Kwanza pombe ile ilimfanya kuwa unstable kisaikolojia na hakuweza kupata usingizi. Mpaka hapa Lashbrook alipata jibu kwamba dawa ya LSD haimfanyi mtu kupoteza kumbukumbu yaani Amnesia.
Sasa vituko vilianza kuonekana asubuhi yake ya jumatatu.
512hupQwlPL._AC_UF1000,1000_QL80_.jpg

Iko hivi siku hiyo bwana Vincent ruwet mtalaamu mwenzake bwana Frank Olson alifika ofisini mwake kwenye kambi ya kijeshi ya fort Detrick na kumkuta Olson akimngojea ofisini mwake akiwa na hali ya mawenge. Na frank akaanza kusema anajisikia kuacha kazi au au afukuzwe tu hajisikii tena kuendelea na kazi(alikuwa psychologically unstable).
Ruwet akamwambia huyu bwana ampe muda afikirie maana ndio alikuwa mkuu wa kitengo alichokuwa akifanya kazi Olson. Kesho yake tena , hivyo hivyo Olson akasema hataki tena kazi na alikuwa kama anaanza kuchanganyikiwa fulani hivi.
Sasa ruwet akaamua kupiga simu makao makuu ya CIA yaliyokuwa Washington kwamba huyu Olson anahitaji medical attention kutokana na hali yake kuwa mbaya. Akamjulisha Robert lashbrook kuhusu kunavyoenda . Kumbuka huyu lashbrook anajua kile kilichokuwa kikiendelea. Ikumbukwe huyu lashbrook alitaka kujua je, hii dawa ya LSD inaweza kumfanya mtu kuchizika na kuanza kutoa siri pasipo yeye kufahamu? Ndio maana aliamua kuchanganya dozi ya LSD kwenye pombe kama test kwa maafisa wa CIA kwa siri pasipo wao kujua.
Sasa ruwet na lashbrook waliamua kumpeleka huyu bwana kwenye matibabu ..
Kwanza walimpeleka kwa daktari mmoja ambaye alikuwa ni mtalaamu wa maswala ya kinga ya mwili na allergy yaani immunologist n allergist aliyeitwa Harold abramson ambaye alikuwa ni mwajiriwa wa siri wa CIA. Lengo kuu la kumpeleka kqa mtalaamu huyu lilikuwa ni kutaka kufahamu kama dawa ya LSD imemuathiri kwa kiasi gani Olson ikiwemo , Kupoteza kumbukumbu au Amnesia lakini bado ilionekana Olson hajapoteza kumbukumbu .kwa kifupi huyu Abramson hakuweza kutambua shida haswa ya Olson ni ipi.

Ruwet na lashbrook wakaamua kumpeleka mwenzao kwa mganga ambaye ni mwanamazingaombwe kwenye mji wa New York aliyeitwa john Mulholland ambaye alikuwa pia kwenye payroll za CIA. Olson alipofika alimweleza kwamba CIA wanataka kumuua na kuna muda anasikia sauti za ajabuajabu kichwani (hallucinations signs) yaani maruweruwe.
Sasa jwa kifupi huyu bwana walikuwa wanaangaika naye ili apate matibabu lakini kiufupi kuzungushwa kote huko ilikuwa wanamfanyia utafiti wa namna sumu ya LSD kama inafanya kazi yake ya kuharibu akili ya mtu kiasi cha kumfanya apoteze uwezo wake na utashi wake wa kiakili.
Sasa mara ya mwisho huyu lashbrook mwenyewe na mgonjwa wake Olson waliamua kupata mapumziko kwenye hoteli ya Statler iliyopo Newyork na wakakodi chumba namba 1018A kilichopo kwenye ghorofa ya 10 kwenye hoteli hiyo. Na usiku huo walipata chakula na vinywaji pamoja (haijulikani kama walikuwa na uhusiano wa kishoga au la🤷🏿). Olson akaamua kupiga simu usiku huo kwa mkeo akimwambia atakuwa Okay soon kisha akaenda kulala.

Ilipofika saa nane na nusu usiku huyu bwana Olson alianguka kutoka chumba alichokuwa amelala kupitia dirishani hadi chini na kufa hapohapo baada ya kupata majeraha kwenye fuvu la kichwa.
Meneja wa hotel hiyo bwana Armand pastore aliposikia kishindo nje akakuta mtu ameanguka kutokea dirisha la chumba cha ghorofani na kumtambua ni Frank Olson.(Haijulikani kama alianguka mwenyewe au alisukumwa )
Haraka alipiga simu na maafisa wa polisi walifika eneo la tukio.
Baada ya hapo walifika hadi chumba alicho book bwana Olson na Lashbrook kwa ajili ya upelelezi. Na wakamkuta lashbrook kutaka kujua kilichojiri. Huyu bwana Lashbrook alikuwa yupo tu toilet akifanya yake na muda huo kabla ya polisi kufika ,tayari alikuwa amewataarifu maafisa wa CIA kwa kilichojiri kwa Olson. Mtu huyo wa CIA alikuwa mkuu wa kitengo cha CIAs Technical service Staff aliyetaarifiwa alikuwa ni Gottlieb ambaye alikuwa anajua ni LSD imefanya kazi dhidi ya Olson.
Huyu bwana Lashbrook alichukuliwa kwa ajili ya mahojiano zaidi na maafisa wa polisi. Lakini baada ya upelelezi CIA waliamua kuizima hii kesi kijasusi maana ilifunguliwa kama Homicide case. Ikazimwa hivyo ikawa imeisha.
Sasa mkasa huu baadaye ulipokuja kugundulika ambapo kipindi hicho CIA ilikuwa chini ya mkurugenzi wake mtata Allen dulles almanusura Shirika hili lisambaratike na baadhi ya project za CIA ziliamua kusitishwa na ikapelekea kashfa kubwa sana enzi hizo kuhusu miradi mingi ya siri ya CIA ambayo ilikuwa kinyume na sheria za kimataifa ikiwemo Nuremberg code.
Subproject22.jpg

Hii ni sehemu ya nyaraka za siri ambazo zilikuwa sehemu ya ushahidi kuhusu project chafu za siri za CIA ikiwemo hii ya Project artichoke au MK- Ultra.
 
Hapana inabidi uiendeleze mkuu hii haijaishia hapo
Upo sahihi.. lakini mada kama hizi ni iwa ajili ya kufunguana kifikra... Nilitamani nianzie mwanzo kabisa ila muda umenibana na kutafuta namna mkono uende kinywani.. sema pia na simu haipo fast sana kwenye kuandika
 
Back
Top Bottom