Frederick Mpendazoe atimkia CCJ...

Mwache aende zake - ameshakuwa "liability" na angebakia CCM "tungempiga chini" katika kura za MAONI!

OFF Topic: TuskerBariiiidi? Siku hizi sikuoni mitaa yetu ya Meeda na B-Bar! Au kwa sababu Tusker imekuwa adimu?

Wow, this is great! Kama kina Mpendazoe ndani ya ccm ni LIABILITY nini kitakachowafanya kina Chenge, Serukamba et al kuwa ASSERTS ndani ya ccm?
 
ninachoamini mimi ni lazima kuwe na gharama ya watu fulani kulipa ili kuleta mageuzi ya kweli nnchini Tanzania, na Mpendazoe analipa Gharama hizo, amejitoa muhanga, ili wengine wenye moyo kama wake wamuunge mkono....huyu anaonyesha sura halisi ya mpinga ufisadi.
uwezi kupinga ufisadi ukiwa chama kimoja na Chenge na Lowassa, huwezi kupinga ufisadi kisha ukamuunga mkono JK, Huwezi kulaani ufujaji wa mali ya umma ukawa chama kimoja na Makamba ....huu ni mwanzo wa Utungu, mapambano ndio kwanza yanaanza.
 
mbona mna haraka jamani.. hata wakitimka watu wengine hawatoamini kwa sababu wamezoea sana geresha. Haya kibereko!!


Kwanza bado kikundi cha sizitaki mbichi hizi lazima kije na kutoa tamko kwamba hata wakiondoka wengine 20,CCM itasimama...ngoja waandishi wa habari wamtafute Makamba au Chiligati usikie.Natamani sana kusikia majibu ya makamba leo hii ,maanake alisema wakitoka CCM watakua wamejimaliza wenyewe
 
Wow, this is great! Kama kina Mpendazoe ndani ya ccm ni LIABILITY nini kitakachowafanya kina Chenge, Serukamba et al kuwa ASSERTS?

Sikujua kwamba wanaopambana na ufisadi ndani ya CCM ni Liability,kwa mawazo haya tuna kazi
 
Well done Mpendazoe! Huu ndio upiganaji halisi. Tupo nyuma yako wewe na wapiganaji wengine watakaokufuata. Saa ya Ukombozi ni sasa!
 
Well done Mpendazoe! Huu ndio upiganaji halisi. Tupo nyuma yako wewe na wapiganaji wengine watakaokufuata. Saa ya Ukombozi ni sasa!
hakika saa ya ukombozi imewadia ....amka Tanzania, amka Tanganyika....Wazanzibar Tayari wameamka na kuukataa udikteta wa CCM Bara, wanaleta sheria kwaajili ya yao wenyewe.
huu ndio wakati wawapinga uchafu wa CCM kuungana , huu ndio wakati wakuwaandalia kina makamba , RA , Lowassa, Chenge kitanzi chao kisiasa...huu ni wakati wakupunguza nguvu zao bungeni.
amka Tanganyika Jogoo ameisha wika.
 


Lakini Tendwa alikuwa sahihi kutamka hayo maana wakati huo ilikuwa ni kabla ya kupelekewa maombi ya usajili. hata mimi ningesema hivyo hivyo kwani CCJ ilikuwa inazungumzwa sana na kuhusisha vigogo wa CCM huku hata maombi ya usajili hayapo mezani kwa Tendwa
 
Nimeanza kuwa na wasiwasi kuhusu CCJ, is it becoming kapu la makapi? Is this Fred Mpendazoe aliyetetea mafisadi kwa nguvu zote, au nimesahau? CCJ ni chama ambacho mtu yoyote anaweza kujiunga bila hata kujua msimamo wa mtu huyo ukoje?

Acha upuuzi wako na ukome kabisa kuwaita wapiganaji wetu makapi.
 
hahhahaha.. miye watu humu wanaboa wakati mwingine.. tumewaandikia humu, watu wametoa na tamko lao, na wametupa hadi Aprili na yote tumewaweka humu watu wanataka watafuniwe hadi washibe ndio wajue wamekula. Ni mwanzo tu...

Mkuu mbona umekuwa mkali hivyo?ni gumu kuamini kuiona CCM ikipasuka...It is so hard to believe.Tumejadili mengi sana humu siyo yote yaliyojadiliwa yametimia mengine yaliishia kujadiliwa tu na hayakluwahi kutokea kuwa kweli ndio maana tunakuwa wakugumu kuamini mpaka tuone na kupapasa.
 
Nani? Mpendazoe? Hakuna kitu huyo. ALikuwa afukuzwe na NEC next week kawashtukia. Hata CCJ watamwona he is a problem. Mtu alimtesa mkewe mapaka akawa mlokole yule mama. Masikini she died about three months ago. Mtaona tu tunayoyasema. Atawasumbua sana. The good news he is a political lightweight wala siyo Kigogo. Halafu CCJ kuja kupata usajili wa kudumu next yeaaar!! Hapo sasa. Mimi naona mahesabu kachemsha. Yaliyomfika Njelu Kasaka na yeye pia atajikuta peke yake.
 
Wow, this is great! Kama kina Mpendazoe ndani ya ccm ni LIABILITY nini kitakachowafanya kina Chenge, Serukamba et al kuwa ASSERTS?

Hope unamaanisha Assets mkuu.....Maana Asserts lina maana nyingine kabisa
 
pole Marigwe, mapambano ndio kwanzaa yameanza, bakieni na kina Lowasa na RA wenu, bakieni na Makamba wenu...chama lenu linanuka ufisadi na ufirauni.
Mbona Rais wako alimuacha mama Ridhwani asijue wapi pa kwenda.
 
hawakuwa na mpango wa kumtimua wala nini; hawawezi kuwatimua wote wenye matatizo na CCM. Na hawawezi kukinyima usajili wa kudumu hata kama wakitaka hawana ubavu huo. Meli imeshaondoka bandarini!
 
hawakuwa na mpango wa kumtimua wala nini; hawawezi kuwatimua wote wenye matatizo na CCM. Na hawawezi kukinyima usajili wa kudumu hata kama wakitaka hawana ubavu huo. Meli imeshaondoka bandarini!
naamini pia hayo maneno Mwanakijiji, kama walikua nania ama hawakuwa na nia swala la msingi ni je kuna maana kwa mwanasiasa makini kukaa chama kimoja na Chenge na RA.....CCM bana.
 
-Yaani wawe na ubavu wa kumtimua Mpendazoe wamwache Rostam aziz au Chenge?wenzetu hawa kwa kugeuza priorities upside down si mchezo,yaani wanavaa hata ndala ya mguu wa kushoto kwenye mguu wa kulia
 
-Yaani wawe na ubavu wa kumtimua Mpendazoe wamwache Rostam aziz au Chenge?wenzetu hawa kwa kugeuza priorities upside down si mchezo,yaani wanavaa hata ndala ya mguu wa kushoto kwenye mguu wa kulia


hahaha.. alimradi wawe wamekubaliana hivyo watadai wanaonesha "umona na mshikamano"
 
Nampongeza zaidi kwa kutobabaishwa na vijisenti hata akaamua kuacha ubunge wake kabla ya kupata hiyo inayoitwa pensheni.
.
Daktari embu nipe mwanga kidogo juu ya hizi taratibu za Bunge. mimi nilikuwa nadhani mfanyakzi wa umma mathalani hata mashirika binafsi akifa wakati wa utumishi wake hulipwa mafao yake yote vivyo hivyo na waheshimiwa wabunge. najua mtu akiacha kazi pia hulipwa mafao yake, Je hili limekaaje kwa wabunge, kwani mheshimiwa ametumika zaidi ya miaka 4 bungeni na ameamua kuacha kwa hiari yake kwanini asilipwe pension sawa sawa na muda aliotumikia bunge??? Tafahdari naomba mwongozo wenu???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…