Frederick Mpendazoe atimkia CCJ...

Frederick Mpendazoe atimkia CCJ...

Anawahi cheo, ila sababu zake za kujitoa CCM kanakiri zile za Mrema za mwaka uleeeee........
 
hahah... kweli mpendazote.............

angalau sasa wafadhili wa CCJ wanaanza kujitokeza.................siamini kama utakuwa uamuzi wa busara............ lakini naamini utajenga demokrasia...................

all the best mpiganaji..............

Mkuu wanaojenga demokrasia nchi hii wanajulikana lakini bwana Mpendazote anajenga domokrasia.Angekuwa mtu asiye-endeshwa na njaa angejitoa CCM mapema sana, siyo kipindi cha uchaguzi.
 
Mwacheni aende atuachie Chama Chetu.

Kama mtu anashindwa kushawiji hoja ndani ya vikao vya chama, na agenda zinapoamuliwa akatika bila kuridhika na kuishia kunung'unika kwenye vyombo vya habari, basi huyo si mwenzetu!

He was a liability, opportunistic and actually a spent force. Kama kuna wengine wenye mtazamo kama wa mwanasiasa huyu, ni bora wamfuate mapema kwani kwenye uchaguzi mkuu watachujwa na hawatapewa nafasi ya kugombea.

Wewe ndio hoi kabisa!! Kuna spent force zaidi ya CCM iliyochosa na kuzeesha watu kiasi hiki? Pole sana!!
 
Mkuu wewe ni mtetezi wa mafisadi ... just in case watu walikuwa hawajakuambia live hapa JF.

Ufisadi ni kutegemea mtu kutetea kila kitu just because unatoka upinzani. Ufisadi ni kumfanya mtu aogope kuongea mawazo yake ili asionekane fisadi. Mkuu just in case sijawahi kukuambia wewe live....I DON'T GIVE A DAMN WHAT YOU THINK OF ME! I call as I see it. Kama ukweli umekuuma pole ndugu.
 
Mkuu wanaojenga demokrasia nchi hii wanajulikana lakini bwana Mpendazote anajenga domokrasia.Angekuwa mtu asiye-endeshwa na njaa angejitoa CCM mapema sana, siyo kipindi cha uchaguzi.

HA HA HA - Wanaoendeshwa na njaa ni mafisadi walioko CCM wanaogombania kuitafuna nchi. Fred angekuwa mlafi angebakia CCM kufanya ulafi.
 
Mkuu wanaojenga demokrasia nchi hii wanajulikana lakini bwana Mpendazote anajenga domokrasia.Angekuwa mtu asiye-endeshwa na njaa angejitoa CCM mapema sana, siyo kipindi cha uchaguzi.

kweli mkuu, yaani amenikers sana kurudia madudu yale yale aliyofanya mrema huko nyuma.......... yaani watu hawajifunzi!!............. sasa ndio asahau kabisa na habari ya ubunge..............
 
Mkuu kama wangekuwa ni wapiganaji wa kweli wa ufisadi wangeondoka CCM miaka kadhaa iliyopita, imebaki miezi michache kwenda kwenye uchaguzi wanajifanya wapiganaji wa kweli. Hakuna kitu nao vile vile ni mafisadi. Wapiganaji wa kweli ni wale wanao chukua hatua mara jambo la kijinga linapofanyika.Mpendazoe alikuwa anatimuliwa soon.

Miaka yote hii wamaekuwa katika harakati za kupigana na mafisadi humo humo ndani ya CCm, lakini sasa wameona kuwa mafisadi hao ni sugu kweli kweli, wanakula na kutapika hapo hapo. Wanajaribu wakiwa nje. Ni another strategy tu.
 
HA HA HA - Wanaoendeshwa na njaa ni mafisadi walioko CCM wanaogombania kuitafuna nchi. Fred angekuwa mlafi angebakia CCM kufanya ulafi.

Huyo Fred ametangaza nia ya kutoka CCM, kwa statement yako hapo juu Fred Mpendazote nae ni fisadi tu.
 
Kwa kanuni zilizopo watamkokotolea mafao yake hadi siku alipoacha ubunge. Hiyo nilikuwa namjibu mwananchi mmoja aliyekuwa anamshangaa huyu bwana kuacha hela za bunge na kwenda upinzani kuliko na umaskini. Hata kama ingekuwa hapati mafao kabisa nadhani sio hoja madamu utashi wake umeamua hivyo.

Kama ndio hivyo nadhani hoja hapa ilikuwa Je, CCJ watapata usajiri wa kudumu? na kama hawatapata nafasi yake ya kurudi bungeni imekaaje?? Kama Uwezekano wa CCJ kupata usajili wa kudumu na kushiriki kwenye uchaguzi mkuu na kama mafao ya wabunge wanaoacha ubunge yapo pale pale, kwanini hao wabungea wasiopenda kinachoendelea ndani ya CCM na wanania ya kujiunga na CCJ wasifanye hivyo sasa? unaweza ukawa ni muda muafaka kuliko kusubiri bunge kuvunjwa at least kea mtazamo wangu
 
Mkuu kama wangekuwa ni wapiganaji wa kweli wa ufisadi wangeondoka CCM miaka kadhaa iliyopita, imebaki miezi michache kwenda kwenye uchaguzi wanajifanya wapiganaji wa kweli. Hakuna kitu nao vile vile ni mafisadi. Wapiganaji wa kweli ni wale wanao chukua hatua mara jambo la kijinga linapofanyika.Mpendazoe alikuwa anatimuliwa soon.

nakuunga mono mia kwa mia.............. mi walipokaa kimya kuhusu richmond.............. niliwadharau wote............. hakika ningekuwa nateua wagombea ubunge nisingeteua hata mmoja wa waliojiita wanapambana na ufisadi, labda ningemfikiria kidogo sendeka............. waliobaki wote ni mafisadi waganga njaa.......... na huyu hata asingetimuliwa, asingepitishwa tena na CCM kuwania ubunge, alishafulia .................

mwansiasa gani amnsimama na hoja moja tu "mkapa na kiwira" miaka mitano, wapiga kura wake hawana huduma yoyote ya maana kutoka kwa mbunge wao!!!!!!!!! mbaya zaidi hoja yenyewe hakuishikilia hadi mwisho, alipoitwa kwenye kamati za chama akanywea, alipogundua awanamtimua karukia chama amabacho hata hakijasajiliwa!!!!!!!!!! busara gani hiii.............. waaasisis wenyewe wa chama wanatafuta huruma za masajili akisajili kabla ya miezui sita inayotakiwa kisheria............. wanaitafuta huruma hii hadi kwa kulia kwenye kaburi la nyerere...............

bora hata angeebda chadema labda ningejitahidi kutafakari kwani anagalau hao walishaeleweka kidogo na watanzania kuwa wanpambana na ufisadi alioushikia bango kwa miaka mitano........... lakini CCJ?......... hata kiitokadi hawaivi................ taifa likiongozwa na watu kama hawa, hakika tutatumbulia wote shimoni..................sijaona hekeima kabisa................
 
Huu ni unafki hakuna lolote

huyu jamaa tangu awali alikuwa anajua kwamba kule jimboni hapati kitu kabisa

sasa anahaha kwa maana ya kuona namna ya kurudi kwenye jimbo

Mpendazoe hongera.

Wesegesege, kama unadhani asingeliweza kupata kitu jimboni kwake basi ni kwa sababu ya kile alichokianika hadharani leo. UFISADI uliokithiri katika ngazi zote za CCM. Kaamua kutumia haki yake ya kidemokrasia, kama hiyo inaweza kumrudisha jimboni yote ni halali yake kama Mtanzania kwa hiyo tuache midomo ya kumpaka matope na kumfanya awe dhalili. Ni shujaa!
 
Mwacheni aende atuachie Chama Chetu.

Kama mtu anashindwa kushawiji hoja ndani ya vikao vya chama, na agenda zinapoamuliwa akatika bila kuridhika na kuishia kunung'unika kwenye vyombo vya habari, basi huyo si mwenzetu!

He was a liability, opportunistic and actually a spent force. Kama kuna wengine wenye mtazamo kama wa mwanasiasa huyu, ni bora wamfuate mapema kwani kwenye uchaguzi mkuu watachujwa na hawatapewa nafasi ya kugombea.

Looser!!!
 
Wanaodhani Mpendazoe kaondoka peke yake naomba waangalie behind the scene wafikirie upya na CCM isipoangalia inaweza kulipoteza jimbo la Kishapu, kwa mwanaCCM makini atasikitika kumpoteza Mpendazoe wasio makini ndio wanaosema bora kaondoka yaani wale wa type ya sizitaki mbichi hizi

Matokeo ya Ubunge Jimbo la Kishapu 2005
CCM
FRED MPENDAZOE TUNGU kura 64,109 sawa na 81.9%
CUF
JUMA MUSSA SHAMTE kura 6,783 sawa na 8.7%
CHADEMA
MAGEMBE KANOGU PAULO kura 6,689 sawa na 8.5%
TLP
SEIF HAMOUD MASELE kura 659 sawa na 0.8%
 
Kwa kanuni zilizopo watamkokotolea mafao yake hadi siku alipoacha ubunge. Hiyo nilikuwa namjibu mwananchi mmoja aliyekuwa anamshangaa huyu bwana kuacha hela za bunge na kwenda upinzani kuliko na umaskini. Hata kama ingekuwa hapati mafao kabisa nadhani sio hoja madamu utashi wake umeamua hivyo.
Kitila,

Naomba toa somo juu ya hili. Watu mbalimbali wanatoa tafsiri tofauti juu ya mafao ya wabunge.

Mimi nilifikiri usipomaliza muda kwa kujitoa au kufukuzwa na chama basi unaambulia sifuri.

Tafadhali tuelemishe!
 
Umekurupuka kuandika hii habari...makosa ya lugha kibaooo...hv umepitia shule ya msingi wewe kweli...but thanks for ur useful post...

Another looser!! Mbona alichoandika kinasomeka na kueleweka?
 
walijaribu kumcontrol jamaa na kumeweka vikao lakini jamaa kachukua msimamo wake. Kama atapoteza ubunge ni gharama ya kuchukua msimamo.. sasa kama hakubaliani na CCM na inavyoendeshwa aendelee kubakia ndani ili awe Mbunge tena?

Hao mbona wako wengi tu ndani ya CCM. Lilipotolewa tamko watu wakataka mbona hawatoki, sasa wametoka watu wanauliza "kwanini wametoka wana nia nyingine" na wakishinda uchaguzi watu watasema sijui vitu gani. Huyu ni mwanzo tu.. hatimaye CCM wataachiwa "wana CCM" halisi.
 
Back
Top Bottom