Fredrick Mchauru - Mtanzania wa kwanza kupata scholarship atimiza miaka 100. Alikuwa Katibu Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Tanganyika

Fredrick Mchauru - Mtanzania wa kwanza kupata scholarship atimiza miaka 100. Alikuwa Katibu Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Tanganyika

Mzee Fredrick Mchauru ambae ni mtanzania wa kwanza kuwai kupata scholarship nchini Tanzania ametimiza miaka 100 leo April 25. Mzee Mchauru alizaliwa tarehe 25 April mwaka 1920 huko Newala Mtwara na alisoma Sekondari ya Chidya na Minaki.

Mzee huyu alikua katibu mkuu katika serikali ya kwanza ya Tanganyika chini ya Rais Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kwasasa makatibu wakuu wa serikali ya Kwanza ya Tanganyika walioko hai ni wawili tu – Mzee Mchauru na Mzee Cleopa David Msuya

View attachment 1430429

Mwaka 1944 Mzee Mchauru pamoja na Mangi Mkuu Thomas Marealle ndio walikua kati ya watanzania wa kwanza kuwai kupata scholarship kutoka kwa serikali ya mkoloni muingereza kwenda kusoma London School of Economics.

Walipofika uingereza walikuta chuo chao kimegeuzwa kua kambi ya wanajeshi wanaopigana vita kuu ya pili ya dunia hivyo walilazimika kwenda kuishi katika chuo kingine huko Birmigham mpaka vita ilipokwisha. Walisoma degree na kumaliza mwaka 1948. Walirudi nyumbani pamoja mwaka 1948 ambapo Mzee Mchauru aliajiriwa kama afisa maendeleo ya jamii mkoani Tabora wakati Marealle aliajiriwa nafasi hiyo hiyo mkoani Morogoro
View attachment 1430491
Mzee Mchauru alikua mume wa Katibu Mkuu wa Zamani wa UWT mama Tecla Mchauru, - aliekua rafiki mkubwa wa mama Anna Abdallah - Mrs Msekwa

View attachment 1430430

Kuanzia mwaka 1962 Mzee Mchauru alifanya kazi kama Principle wa kwanza wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru. Mwanzo chuo hiki kilijengwa kama Polish refugee camp yaani kambi ya wakimbizi wakipolish wa vita kuu ya dunia.

Wakimbizi hao wapolish walifungua ranch ya mifugo hapo Tengeru ambayo baadae ilibadilishwa n akua Chuo cha Tengeru ambacho kipo mpaka leo. After the refugees departed, the government used the site to develop an agricultural research station with soil conservation services. The Game Department was also added to the site.

Picha hapa chini inamuonyesha Mzee Mchauru akiwa Principle wa Chuo cha tengeru akimsikiliza naibu waziri alietembelea chuo hicho mwaka 1962 mama Lucy Lamerk

View attachment 1430431

Baada ya Uhuru mwaka 1965 Mzee Mchauru alichaguliwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kua Katibu Mkuu wa iliyokua Wizara ya Ustawi wa jamii, Ushirika na Utamaduni.

Wakati huo Serikali ya Mwalimu Nyerere ilikua na Makatibu Wakuu 19 chini ya Chief Secretary Joseph Augustine Namata. Makatibu wakuu hao walikua Bwana Dunstan Alfred Omari, Dan Nkembo, Paul Sozigwa, the two Mulokozi’s –Bernard Kyaruzi and his brother Dr. Vestadus Kyaruzi, Cecil Kalaghe, Cleopa Msuya, Obed Katikaza, Amon Nsekela, Dr. D. Mtawali and Chief Mwinamila Lukumbuzya. The Attorney General was Mark Bomani
View attachment 1430432


Pichani hapa chini Mzee Mchauru akiwa na Waziri wa Ulinzi bwana Edward Sokoine na rais wa Korea bwana Kim IL Sung (wakati kati)

View attachment 1430433


Picha ingine hapa chini ikimuonyesha mzee Mchauru akisalimiana na waziri mkuu wa china bwana Chou Enlai huko China mwaka 1972

View attachment 1430434

Baada ya hapo Mzee Mchauru aliteuliwa kua Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Ndani ya nchi toka mwaka 1968 to 1971 akifanya kazi na IGP Elangwa Shaidi & Hamza Aziz (Hamza Aziz ni kaka wa Dossa Azi – wote ni Watoto wa Aziz Ali aliekua anamiliki eneo lote la Mtoni kwa Aziz Ali estate). Pichani hapo chini Mzee Mchauru na IGP Elangwa Shaidi wakimsikiliza rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume


View attachment 1430435

In 1972 President Julius Kambarage Nyerere established the Ministry of Defence and National Services and Mchauru was appointed to become its first Permanent Secretary and Hon. Edward Moringe Sokoine as its Minister.

Mzee Mchauru retired government services in 1973 and become either adviser or Board Member to several government and private entities. Aliwai kua Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta na Simu na Shirika la Geita Gold Mines Ambalo baadae lilikuja kua Ashanti Gold Mine (mashirika haya yalianzishwa kwa ushirikiano wake yeye na Mr Niven Sinclair wa uingereza – pichani hapo chini)

View attachment 1430437

Pichani hapo chini Mzee Mchauru akiwa kwenye sherehe ya kumuaga IGP Elangwa Shaid na Kumkiribisha IGP Hamza Aziz watatu kutoka kulia

View attachment 1430438

Mzee Mchauru is a true statesman and a civilian servant who worked for the colonial government and the free Tanganyika all his life. He worked for the government for 26 years from 1947 to 1973 and continued on as an advisor and board member to private & government institutions for another 26 years from 1973 to 1999 making a total of 52 year of service and excellence.

This autobiography is an extraordinarily candid portrait of a humble man who decided early in life to devote his life & intellectual gifts, and his astonishing capacity for hard work, to serving his country.

Indeed, the life and times of Mzee Fredrick Mchauru is the life and times of Tanzania First Phase Government of Mwalimu Nyerere.

Kwasasa Mzee Mchauru anaishi na familia yake jijini Dar es salaam huko Upanga Magharibi Mtaa wa Kitonga Plot 121 nyuma ya hospitali ya Tumaini.

Happy Birthday babu, happy birthday baba. Tunakuombea Maisha marefu zaidi yenye afya na fanaka.. Hakika tunayo kila haki ya kumshukuru Mungu kwa upendo wake mkuu
Principal ndiyo neno sahihi sio Principle
 
Hongera kwake mzee Mchauru...
Ni MTANGANYIKA wa kwanza sidhani hata Tanzania ilikuwepo kwenye mawazo ya wakoloni wakati akienda masomoni..

Everyday is Saturday.........................😎
 
Hongera kwake mzee Mchauru...
Ni MTANGANYIKA wa kwanza sidhani hata Tanzania ilikuwepo kwenye mawazo ya wakoloni wakati akienda masomoni..

Everyday is Saturday.........................😎

Absolutely
 
Back
Top Bottom