Fredy Koublani ni mchezaji mzuri sana akitumiwa vizuri ataisaidia sana SIMBA SC atafanya maajabu NBC PL.

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Mimi naomba nitofautiane kidogo na wadau wengi wa jukwaa hili hasa hasa wana YANGA wenzangu na mashabiki wa simba SC wanaodai Fredy Koublan ni garasa.

Huyu mchezaji namfananisha na the great khali (kwa walioangalia mieleka miaka ya 2005 watakua wanamjua vilivyo)
Ana mwili mkubwa, ni mrefu, ameshiba pia ana nguvu ni kama the great khali ambaye ushindi wake WWE huupata kwa advantsge ya umbo lake na mwili wake, mbinu na ufundi sifuri, akikutana nakimtu chenye mwili mdogo kama andunje chenye mbinu alikuwa anapigwa vizuri kabisa japokuwa sio mara zote kijamaa kinaitwa REMYSTERIO si mnakikumbuka?

Fredy huwa anasumbua sana mabeki akiwa na mpira ni ngumu kumpokonya maana ananguvu kama kifaru ila hana skills nzuri za kufunga, hupenya kirahisi ndani ya 18 na ni vigumu kumpiga .mtama au kumpush akaanguka, ili kumuwini inabidi akabwe na watu wanne azingirwe pande zote. Beki kitasa BACCA alimshindwa akatufunga, magoli mengi anayofunga ni ya kuwashinda nhuvu mabeki.

Ushauri wangu huyu mwamba achezeshwe namba 10 kwa sababu hiyo namba inahitaji mtu mwenye misuri na anayeweza kupenya kirahisi ukuta wa beki zote za kati na pembeni,

Atafutwe namba tisa mwingine mwepesi mwenye mbio

Simba itapata matokeo ya haraka

NAWASILISHA
 
Mieleka ni mchezo wa maigizo kama kaole, kumfananisha tu na wacheza mieleka tayari ushamvua nyota.
Hiyo tunaita kufikiria kwa imagination, kwani wewe nikikufananisha na PROFESSOR wa LACASA DE PAPEL haimainishi kuwa ni series ya ukweli sio fiction bali ntakuwa najaribu kuwasilisha wazo kwa kutumia mfano wa kufikirika ili kufikisha ujumbe
 
Wakati wanakuja Fredy na Jobe Mechi za mwanzo niliona jobe mzuri kuliko Freddy ila baadae ndio nimegundua Freddy yuko vzr
 
Wakati ukifika nitakuja kukumbusha
 
Reactions: Tsh
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…