Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kuwa ajali ya treni ya Mjini kwenda Pugu, iliyotokea Stesheni ya KAMATA kwenye makutano ya reli na Barabara ya Kawawa, jana Mei 13, 2025 imejeruhi Watu 10
TRC imesema ajali hiyo iliyohusisha mabehewa 12 yaliyobeba abiria takribani 1,200 na kuwa Wataalamu wa Shirika na Timu ya Afya ya Shirika, walifika kutoa msaada wa huduma ya kwanza, waliojeruhiwa wawili ni Wanaume na nane Wanawake walikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Amana.
Alichozungumza Afande Sele kiko hapa ~ Afande Sele: Utaratibu wa kutoka Kituo cha SGR - Morogoro haufai, unachelewesha Watu na unachosha abiria
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa TRC, Fredy Mwanjala anaelezea kuhusu ujumbe huo:
Anasema: “Baada ya JamiiForums.com kuichapisha video fupi ikimuonesha Msanii wa Bongo Fleva, Seleman Msindi (Afande Sele) akitoa wito kwa Mamlaka kuweka utaratibu mzuri wakati wa kutoka katika Kituo cha Treni ya Mwendokasi SGR Mkoani Morogoro, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeelezea kuhusu eneo hilo.
“Tumeona video ya Afande Sele akielezea changamoto katika Kituo cha SGR Morogoro, ukweli ni kuwa siku ambayo alirekodi hiyo video kulikuwa na changamoto ya magari wakati wa kutoka na sio kwamba siku zote hali ipo hivyo.
“TRC imeweka utaratibu mzuri na ndio unaoendelea mpaka sasa kinachotokea ni kuwa baadhi ya madereva wanashindwa kufuata utaratibu wakati wa kutoka na wao ndio chanzo cha kusababisha usumbufu na foleni mara moja moja.
“Unaweza kukuta dereva ambaye ni abiria au mtu mwingine anaofika kituoni hapo, akiwa kwenye foleni ya kutoka, anatoka ndani ya gari anaenda kulipa bila kufuata utaratibu, chombo chake alichokiacha kwenye foleni kinasababisha usumbufu au kinaongeza foleni kubwa zaidi.
“Hivyo, tunatoa wito kuwa Watu wafuate utaratibu wakati wa kutoka, Shirika limeweka mazingira mazuri lakini baadhi ya Watu ndio chanzo cha foleni lakini so far kwa sasa kila kitu kipo vizuri.”