Freedom in the World 2018: Democracy in Crisis (Uhuru, Demokrasia na Haki za Kibinadamu)

pingli-nywee

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
11,923
Reaction score
13,350
Hii ni ripoti ya kila mwaka, ya shirika la kimataifa la Freedom House. Kuhusu uhuru, demokrasia na haki za kibinadam duniani. Hizi hapa ni nchi kumi zinazoangaziwa kwa kuminya demokrasia, kukandamiza wanahabari na kukiuka haki za kibinadam na sheria za nchi. **Viashiria vya hali inavoendelea kwenye nchi hizi hapa juu ni hizo 'Trend Arrows': Nyekundu- hali inaendelea kuwa mbaya. Kijani kibichi- kuna afueni kiaina.** Hizi nazo ni nchi kumi na mbili 'worst of the worst' kwenye masuala ya uhuru, demokrasia na haki za kibinadam. https://freedomhouse.org/report/freedom-world/freedom-world-2018 Utafiti huu umetumia 'freedom rating' ambayo inajumuisha 'political rights'(haki na uhuru kisiasa/demokrasia) na 'civil liberties'(uhuru wa wananchi/wanahabari kwenye masuala mengine kama haki ya kujieleza).
 
Asante walau Afrika tumewakilshwa, kwanza EAC tupo humo, ndugu zetu wa kusini wametuwakilisha moja kwa moja........wazee wa "kama unabisha nyanyua mkono au jifanye unajikuna".
 
Utafiti huu kwenye ripoti yenyewe, Freedom in the World 2018: Democracy in Crisis, umeashiria kwamba kwa miaka kumi na miwili, hadi sasa, uhuru, demokrasia na haki za kibinadam zimekuwa zikidorora kila uchao. Nchi 71 zimekuwa kwenye 'decline' mwaka huu, huku nchi 35 pekee yake zikibadilika kuelekea kwa hali iliyo nzuri. Chanzo cha haya yote kwa maneno yao ni, emboldened autocrats, beleaguered democracies. Yaani kuchipuka kwa viongozi miungu watu na demokrasia finyu zisizo na muelekeo. Wametaja pia kwamba, totalitarianism of pre-cold war era is back(ubabe wa enzi zile za baada ya nchi za Afrika kupata uhuru). Uchaguzi kubatilishwa na mahakama Kenya umetajwa kama point ambayo Kenya ilirudi kwenye njia ifaayo baada ya uchaguzi uliokuwa na utata. Huku Uganda ikiangaziwa kwa kutumia sheria ya uhaini na kufunga mitandao ya kijamii. Tz, kuwatia mbaroni wananchi kwa kujieleza mitandaoni, kukandamiza upinzani na kuwatupa korokoni viongozi kutoka kwa vyama vya upinzani, kufunga mashirika ya habari.
 
Asante walau Afrika tumewakilshwa, kwanza EAC tupo humo, ndugu zetu wa kusini wametuwakilisha moja kwa moja........wazee wa "kama unabisha nyanyua mkono au jifanye unajikuna".
Haaa! [emoji15] Eti jifanye unajikuna, hivo ndio kunaendaga?
 
Teh teh teh tihiii
read #1 Bolivia criterion, then compare with what is happening in Uganda.

Ahaaa haaa haaa
you will see how fake is your source.
Acha blah blah zako wewe. Fake wakati ni shirika huru ambalo data zake zinatumika hadi na Human Rights Watch na UN Human Rights Council pia?
 
Acha blah blah zako wewe. Fake wakati ni shirika huru ambalo data zake zinatumika hadi na Human Rights Watch na UN Human Rights Council pia?

Teh teh teh tihiii
za kuambiwa changanya na ZAKO.

Ahaaa haaa haaa
swali langu.
angalia Bolivia na Uganda kama kuna tofauti
 
Teh teh teh tihiii
za kuambiwa changanya na ZAKO.

Ahaaa haaa haaa
swali langu.
angalia Bolivia na Uganda kama kuna tofauti
Aisee, nimekuekea link hapo, Uganda pia imetajwa ila status yake haijapanda wala kushuka, nimeeleza kidogo hapo kwenye comment yangu #6. Alafu mbona hutaji nchi yako? Nalendwa njoo tafadhali unisaidie kutafsiri.
 
Aisee, nimekuekea link hapo, Uganda pia imetajwa ila status yake haijapanda wala kushuka, nimeeleza kidogo hapo kwenye comment yangu #6. Alafu mbona hutaji nchi yako? Nalendwa njoo tafadhali unisaidie kutafsiri.


Ngumu kumeza Jirani.
The bitter truth! 😀
 
Write your reply...
mambo ya jiwe hayo.. ila hili lijamaa mi nalikubali sana!
 
ngoja waje waione hio statement..kisha ifikie kim jong-un....JF itafungwa kwa miezi miwili...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…