Freelancing: Leo nimepata order/kazi yangu ya kwanza kama freelancer!

Miaka miwili iliyopita nilisikia kwa mara ya kwanza juu ya freelancing na kwa kumbukumbu zangu ilikua hapa hapa JF kule kwenye jukwaa la ajira (too bad nimemsahau aliyeleta ule uzi)!
Inawezekana ikawa ni ndugu GLOBAL CITIZEN

My take.
- Hongera kwa hatua kubwa.

- Mawasiliano: Boresha mawasiliano yako kwa kujibu wateja kwa wakati, Download hii SPIKE app: Spike: More than email. Better than chat. - Apps on Google Play
Weka email yako unayotumia, na hakika itakusaidia kuona jumbe (email) kwa haraka na utaweza ku_chat nao kama katika email kama msg za kawaida.

- Uwanja wa freelancing ni mpana, paka maarifa zaidi kwa kupitia makala za GLOBAL CITIZEN hapa: https://www.jamiiforums.com/search/5168419/ utaona ni jinsi gani jamaa anavyo pambana na ametoa tips and tricks nyingi za kuhakikisha unapata kazi nyingi kwa site tofauti tofauti.
 
Mwl.RCT,

Shukrani sana mkuu.

Nafurahi watu wanaanza kupata kazi kwenye site za freelance.

Huu ni mwanzo tu.

Watu wataendelea kupata kazi na kujiongezea kipato.

Kwa mfano mimi kwasababu ni verified member UpWork na pia Freelancer huwa natumiwa job offers hata kabla freelancer wengine hawajaziona



Hii hapa chini ni moja ya project ninayoendea nayo $1000+




Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Piga kazi aisee, mdogo mdogo ndio mwendo , cha muhimu ni Trust na Skills ( uwe nazo nyingi uwe multi purpose aka uwanja mpana ) , cash itakuja yenyewe

Binafsi najuta kwa nini nilichelewa kujiunga, well nna miaka kama 3 tu tangu niingie freelancing , na hii ni kwa jana pekee


 
Mkuu tupeane muongozo wa namna yakufanya hizo kazi na je anaitajika mtu wa level gani ya elimu

$ There's clear light at the end of the Tannel $
Inategemea na kazi, mfano huwezi fanya kazi za ku design majengo kama wewe sio injinia.

No one cares una level gani ya elimu kapo ukiwa na level flan inaweza kuwa faida kwako.

All in all ukishajua english tayari una chance.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Freelancer ni pagu aiseh competition nyingi sana na wahindi wapo kibao huko mi fiverr ndio chaguo langu at least kwa mwezi sikosi USD 300 tupeane maujanja kwa wale wanaopata oder kwenye mtandao wa freelancer

Sent using Jamii Forums mobile app
Penye nia hapakosi njia mkuu!! Kweli ushindani upo lakini inawezekana!!
 
Upepo wa Pesa, Naomba kufahamu mpango wa malipo unafanikiwa kwa kutumia njia gani mkuu? Najua zipo njia kama paypol ila sijui unajiungaje hadi pesa inakukuta

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemea na mtandao unaotumia, kuna websites zinatumia bank transfer, paypal! ila naona njia rahisi ni bank transfer na kutumia payoneer online bank ambayo wanatoa na mastercard kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…