Anaandika Absalom Kibanda
Katika hili kundi lililofungiwa sina cha kuficha hata kimoja. Usitumie moyo au ulimi kufikiri.
Jeuri na nguvu ya CHADEMA leo ni matokeo ya kazi ya kutukuka ya Freeman Aikaeli Mbowe.
Mkwamo wa Chadema leo unatokana na Mbowe kukumbatia sana makosa ya Lissu na wasaidizi wake kwa manufaa ya Chadema, lakini leo yeye ndiye anapigwa. Chadema imejitoa katika maridhiano kwa sababu ya Mbowe kukubali kutekwa na akina Lissu. Yote haya ni matokeo ya makosa ya kujutia huyo huyo Freeman Aikaeli Mbowe.
Jeuri, kiburi na hata uzima wa Tundu Antipasi Lissu ni matokeo ya uongozi mahiri wa Freeman Aikaei Mbowe.
Mashabiki na maadui wa Freeman Aikaeli Mbowe leo walio ndani na nje ya CHADEMA leo ni zao la uongozi wa Freeman Aikaeli Mbowe.
Mbowe ni kiongozi shupavu na mjenzi, Lissu ni mwanaharakati machachari. Mbowe ni mbunifu, Lissu ni zao la ubunifu wa Mbowe.
Unaweza kumfananisha Mbowe na Mwalimu Nyerere katika kujenga chama au na Nelson Mandela kwa kujitoa kwa ajili ya watu wake.
Unaweza kumfananisha Lissu na Chris Hani kwa misimamo
Mikali au Christopher Mtikila kwa upambanaji na zaidi Augustine Mrema kwa kushabikiwa.
Unao uhuru wa kuchagua
Update..1
Naweka hapa hii Comment ya MwanaJamii Forum kuhusiana na habari hii
Mambo 6 yaliyoibuka kuhusu uchangiaji wa mashabiki wa Tundu Lissu baada ya andishi la Mwanahabari nguli Absalom Kibanda.
1. Mwandishi ameongea ukweli unaowauma mashabiki wa Lisu. Wanajua kuwa Lisu amekuwa hivyo alivyo leo kwasababu ya Mbowe "kumvumilia makosa yake mengi" lakini hawataki kukubali kwasababu wao wanaamini Lisu ni bora sana kuliko Mbowe kwasababu anaongea zaidi
2. Wachangiaji wengi wanapenda ushabiki na kwasababu ni mashabiki wanadhani ni rahisi kusema "iwe hivi" na ikawa hivyo muda huo huo kama Mungu alivyoumba dunia na vilivyomo kwa kutamka. Kila anachosema Lisu wao wanakipokea na kukimeza wakidhani ni rahisi rahisi kama anavyokitamka. Tusubiri mwakani tuone "No reforms No election" itakavyotekelezeka
3. Wanaamini Lisu ataiamrisha serikali na kila atakachoamrisha kitatekelezwa na serikali tena bila kuchelewa. Wasichokijua ni kwamba Lisu mwenyewe anajua kuwa hilo haliwezekani
4. Hawaelewi kuwa Lisu ni mwanaharakati na kazi ya mwanaharakati kila siku ni kuongea na kuwajaza matumaini wanaomshabikia. Akishaongea na kuwajaza matumaini "hewa" wanaomshabikia amemaliza kazi yake
5. Wanashindwa kutofautisha kati ya kampeni za kutaka uongozi na kampeni za kutaka kukubalika zaidi kuliko mwingine. Kiongozi bora haombi kuungwa mkono kwa kumsema mwenzake bali kwa hoja na mikakati bora zaidi ya mwenzake
6. Walitamani Lisu aachwe agombee peke yake