Freeman Mbowe alalamikia Uhamiaji uwanja wa ndege Nyerere kwa kumsumbua Mtoto wake ambaye ni raia wa Marekani kuingia nchini

Freeman Mbowe alalamikia Uhamiaji uwanja wa ndege Nyerere kwa kumsumbua Mtoto wake ambaye ni raia wa Marekani kuingia nchini

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Akiwa Marekani akiongea na Watanzania waishio Marekani akisema mtoto wake wa kumzaa aliyezaliwa Marekani na mwenye uraia wa Marekani alisumbuliwa Airport Dar kwa saa sita na kuzuiwa kupewa visa ya kuingia nchini hadi ikabidi aondoke aende Kenya ambako aliingia nchini kupitia Mombasa.
 
Kuna jambo pengine wengine hamfahamu. Ukiwa na mwanao anasoma nje ya Tanzania hasa ulaya na marekani wakati anaingia huko akiwa na miaka chini ya 18 anakuwa minor hibyo yupo kwa uraia wa mama. Akifikisha miaka 18 anauwezo wa kubadili uraia wake. Na watu wengi wamekuwa wakifanya hivyo kwa lengo la kupata favour ya wenyeji mfano unafuu wa ada na utafutaji wa kazi.

Hivyo sio jambo la kushangaza tumeona hata mtoto wa Rais wa George Weah wakati wa kombe la Dunia akiichezea marekani badala ya taifa la baba yake.
 
Uhamiaji wanafanya kazi zao kwa mazoea ya kizembe sana, juzi nimeona twitter watalii wamekalishwa uwanja wa ndege muda mrefu bila sababu yoyote ya maana, ajabu kule nje mnatangaza royal tour, kisha wakifika ndani hamjui kuwapokea!.
Uwanja wa ndege,machine zote za kuscan passport hazifanyi kazi muda tu....
Passport zote zinakaguliwa manually mzee

Ova
 
Huyo mtoto ni raia wa nchi nyingine inabd afate utaratibu,
Si umeambiwa ana uraia wa Marekani?!

It means aliingia kama Mmarekani, na kwahiyo alifuata utaratibu kama Mmarekani.

Lakini kwavile Uhamiaji walifahamu kwamba ni Mtoto wa Mbowe, hawakutaka tena kum-handle kama Mmarekani bali kama Mtoto wa Mbowe!

Na Tanzania tunazo nchi ambazo raia wake wanaweza kupata visa on arrival, na moja ya hizo nchi ni Marekani.
 
Kama ni kweli alifanyiwa uhuni angeripoti kwenye ubalozi wao wa Marekani. Huwezi kuwafanyia uhuni raia wao kwa sababu za siasa zetu hizi chafu.
 
Back
Top Bottom