- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Limeandika Gazeti la Nipashe kuwa Mbowe amemtuhumu Lissu kuhusika kwenye kifo cha Mzee Ali Kibao. Taarifa hii ina ukweli?
- Tunachokijua
- Freeman Mbowe ni ni mwanasiasa maarufu nchini Tanzania. Yeye ni kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini.
Tangu itokee taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu Ally Mohamed Kibao kumeibuka shutuma nyingi kutoka pande mbalimbali nchini zikiwahusisha watu mbalimbali kuhusika na mauaji ya kiongozi huyo..
Mnamo Septemba 11, 2024 kumeibuka taarifa yenye picha na nukuu ya Gazeti la Nipashe inayodai kuwa Freeman Mbowe anamshutumu Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kuhusika na kifo cha Mzee Kibao.
Je, kuna ukweli kwenye taarifa hiyo?
Uchunguzi wa JamiiCheck kupitia pitio la kimtandao limebaini kuwa taarifa na nukuu hiyo si ya kweli. Uchunguzi wetu umeonesha majibu kuwa taarifa hiyo imetengenezwa na kutumia rangi na kupachikwa jina la Nipashe ili kuifanya taarifa hiyo iendane na machapisho ya Nipashe. Aina ya Mwandiko (font) iliyotumika kutengenezea chapisho hilo haifanani na font inayotumiwa na Nipashe katika kuchapisha taarifa mbalimbali katika kurasa zao.
Pia, JamiiCheck imechunguza kurasa rasmi za mitandao Nipashe ambapo yote haikuwa na hiyo taarifa hiyo. JamiiCheck imewasiliana na Mhariri Mtendaji wa Nipashe, Beatrice Bandawe ambaye amesema:
Hiyo taarifa siyo ya kwetu na haina uhusiano na Gazeti la Nipashe wala Nipashe Digital.
Zaidi ya hayo, Uchunguzi wa JamiiCheck umebaini kuwapo kwa taarifa kama hiyo pia katika Mtandao wa X (imehifadhiwa hapa) inayomshutumu Lissu kuhusika na kifo cha Mzee Kibao ikiwa imetengenezwa na kufanana na machapisho ya The Chanzo. Tazama hapa Chini:
Taarifa inayohusishwa na The Chanzo
JamiiCheck imepitia kurasa zote rasmi za The Chanzo ambao wameweka andiko maalumu kukanusha taarifa hiyo (lisome hapa). Katika chapisho hilo The Chanzo wameandika:
Hizi jumbe zinazosambazwa na kurasa mbalimbali za mtandao wa X, ni habari za potufu ambazo hazihusiani na The Chanzo. Habari zetu zote zinapatikana kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii na tovuti yetu.