Freeman Mbowe: CCM wanakusudia kutukatisha tamaa na sisi wakati mwingine tunawehuka na kuanza kukata tamaa

Freeman Mbowe: CCM wanakusudia kutukatisha tamaa na sisi wakati mwingine tunawehuka na kuanza kukata tamaa

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Freeman Mbowe akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi ya CHADEMA wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Jumapili Desemba 15, 2024.

Updates...

Mbowe

CHADEMA inaoutofauti na vyama vingine vya upinzani kwa sababu kimeweza kuimili misukosuko kwa sababu kimejengwa ndani ya mioyo ya wana CHADEMA na ukiwaona kimejengwa kwenye mioyo ya wana CHADEMA.

Ninapenda kuchukua nafasi hii kuwapa pole sana wapiganaji wote mlioko mahali hapa ambao mlikuwa wagombea wa serikali za mitaa katika maeneo yetu ya Jiji letu la Dar es Salaam, kanda ya Pwani na hata wale wote waliojitokeza nchi nzima. Rai yangu kama Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, kosa kubwa sana katika maisha ya binadamu na katika harakati ni kukata tamaa. Hawa wenzetu wa upande wa pili (CCM) wana kusudio la makusudi kabisa kabisa la kutukatisha tamaa, na sisi wakati mwingine tunawehuka na kuanza kukata tamaa na kuona kuwa safari yetu haiwezekani"

"Nimesema na ninarudia tena, kitendo cha serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kusimamia wizi wa kura mchana kweupe, una mambo mawili. Kwanza ni kukiri udhaifu wao wa kupambana kwenye sanduku la kura kwa misingi ya kweli na haki, ni ushuhuda tosha kuwa wenzetu hawajiamini tena kwenye sanduku la kura. Jambo la pili, ni ushuhuda ulio wazi kwamba wenzetu hawa wanaihofia CHADEMA kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya mageuzi ya vyama vingi katika nchi yetu.

Ndiyo sababu watu wazima na busara zao, wanakubali fedheha ya kutukanwa na kudharauliwa nchi nzima kwa wizi wa kura unaofanyika mchana ambao kila binadamu mwenye akili timamu anaona. Ukiona mtu wa aina hiyo anakubali aibu ya kiwango hicho ujue mtu huyo amefika kiwango cha chini kabisa kabisa cha ujasiri wa kisiasa. Kwahiyo nyinyi badala ya kukata tamaa, mnapaswa kujikusanya na kujitafakari, tuchambue tulikosea wapi. Ndiyo, tumeonewa lakini kwanini tumeruhusu tukaonewa namna hii? Tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu ujao, ofisi hii kuanzia kesho (Desemba 16, 2024) ikageuke kuwa eneo la mkakati wa namna ya kuandaa Kinondoni kufikia malengo yetu ya kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao

Si mlituambia anatangaza Nia.
 
"Nimesema na ninarudia tena, kitendo cha serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kusimamia wizi wa kura mchana kweupe, una mambo mawili. Kwanza ni kukiri udhaifu wao wa kupambana kwenye sanduku la kura kwa misingi ya kweli na haki, ni ushuhuda tosha kuwa wenzetu hawajiamini tena kwenye sanduku la kura. Jambo la pili, ni ushuhuda ulio wazi kwamba wenzetu hawa wanaihofia CHADEMA kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya mageuzi ya vyama vingi katika nchi yetu.
Nani aliyekwenda kunywa juice na namba 1 wao? Tuanzie hapo
 
Itakuwa demokrasia.

Isipo it’s time ya Mwenyekiti wenu ku retire kwa sheria za nchi 60+ years ni muda wa kulea wajukuu.
Mbona CCM wana waziri ambaye anakaribia miaka 80?! Kwa nini naye asijiuzulu?!
 
🐼

Haya

J J Mnyika ana Press Kesho saa 5

Kambale clan
HIyo inaweza kuwa clan bora zaidi yenye kutoa protain na calcium kwa wingi kuliko Panya clan isiyo na manufaa kwa binadamu zaidi ya kuwa lishe ya mnyama anayefugwa na binaadamu.
 
Iwapo unayosema ni kweli kondoo wajiandae kwenda kutafutwa msitu wa Shakahola kwa akina Mackenzie
imeandikwa....

Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana kondoo wangu.”:pulpTRAVOLTA:

Yohana.21:15
 
Ila sii msituni
 
Back
Top Bottom