Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, ameibukia Kanda ya Kaskazini kwenye kikao cha kazi, siku chache baada ya uzushi wa tukio la kupewa sumu. Katika hotuba yake, Mbowe alikumbusha dhamira ya kuanzishwa kwa chama hiki miaka 33 iliyopita, akisisitiza kuwa malengo yao ni makubwa kuliko changamoto zinazowakabili.
“Wakati wote tukikumbuka dhamira ya kuanzishwa kwa chama hiki, lazima iwe kubwa kuliko kutekwa kwetu, kupoteza mali zetu na kupoteza fursa yoyote. Licha ya yote tuliyoyapitia, sote tulisimama na leo tumekuwa mashujaa,” alisema Mbowe, akionesha imani katika nguvu ya chama chake.
Akiweka wazi hali ya kisiasa nchini, Mbowe alisisitiza kwamba ukuaji wa CHADEMA unachangia mivutano ya kisiasa. “Utomvu wa nidhamu ni madhara ya kukua; ukiona chama cha siasa hakina mivutano, hicho ni chama mfu,” alisema. Aliwakumbusha wanachama wa CHADEMA kuwa, tofauti na vyama vingine vilivyoshindwa, wao wamechagua kusimama imara, badala ya kukata tamaa.
Pia, Soma:
-> CHADEMA Kufanya Mikutano 105 kwa siku 21 tu Kanda ya Kaskazini, Lissu na Mbowe kuongoza Mashambulizi
-> Mbowe: Kuna Watu wanasema Nina mgogoro na Tundu Lissu nawaambia Watasubiri sana, Chopa inaanza operation Karatu na Nitakuwa na Tundu Lissu!
-> Mbowe: Siwezi gombana na Lema, mama yake atanipigia Simu
-> Freeman Mbowe mwanasiasa, mfanyabiashara na mkulima asiye ogopa hasara