Freeman Mbowe kuhamia CCM, CHADEMA inaanguka?

Freeman Mbowe kuhamia CCM, CHADEMA inaanguka?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
WanaJf,
Salaam!

Zipo dalili nyingi za mtawala wa milele ndani ya CHADEMA kuhamia CCM. Dalili hizi ni:

(a). Mbowe kukubali msamaha wa kuachiwa huru baada ya kupiga magoti CCM - alifutiwa mashitaka mazitomazito;

(b). Mbowe kukubali kwenda kula futari na kunywa Juice iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa;

(c). Mbowe kukubali ruzuku wakiyoikataa tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020;

(d). Mbowe kuwakimbia kundi la wabunge wa Covid 19 - wanaopata uhalali kupitia MAHAKAMA.
CHADEMA sasa mahututi mbowe akikimbia. CCM kulamba dume.
 
Mbowe hawezi kuhamia CCM kamwe. Atakuwa ni mjinga mno kuachana na mali yake binafsi inayomwingizia mamilioni ya pesa kupitia ruzuku na michango mbalimbali ya wanachama (nyumbu) na wafadhili. Pia kutelekeza mali ya urithi toka kwa baba mkwe inaweza kumletea laana.

Na kwa upande mwingine itakuwa sio sawa upinzani kufa kabisa... Mbowe abaki CHADEMA kimkakati. Anaweza kuisaidia CCM akiwa hukohuko CHADEMA.

Tayari tumeshaona jitihada zake... kwa maelekezo yake tumeona kina Lema wakitukana wapiga kura (bodaboda na kina mama wa VICOBA) ili kukikosesha CHADEMA kura 2025.
NAMPONGEZA SANA MWENYEKITI WA KUDUMU MH MBOWE.
 
Probably matokeo yake hayatabiriki ila naweza kuongelea katika nukta hizi,

Kuondoka kwake huenda CHADEMA ikafanikiwa zaidi ya apo ilipo coz ukiongelea Chama unaongelea misingi na muundo(SHERIA, utaratibu, katiba, structure ya uongozi) hivyo vyote vitabaki huyo Mbowe akiondoka kwani hata CCM ilikuwa inaongozwa na Nyerere akaja Mwinyi mpk kufikia Samia Hassani.

Nukta ya pili akiondoka Chama Kinaweza kufa,Miaka takribani 10 amekiongoza Chama kama Mwenyekiti na amepitia mengi,anakijua Chama in-out hivyo waswahili wanaswma zimwi likujualo halili likakwisha.
 
Wahuni bwana, eti wanasema kile cheo ni chao kanda ile toka enzi za Nyerere, ngoja tuone siasa za saigon. Time is the best doctor.
 
WanaJf,
Salaam!

Zipo dalili nyingi za mtawala wa milele ndani ya CHADEMA kuhamia CCM. Dalili hizi ni:

(a). Mbowe kukubali msamaha wa kuachiwa huru baada ya kupiga magoti CCM - alifutiwa mashitaka mazitomazito;

(b). Mbowe kukubali kwenda kula futari na kunywa Juice iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa;

(c). Mbowe kukubali ruzuku wakiyoikataa tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020;

(d). Mbowe kuwakimbia kundi la wabunge wa Covid 19 - wanaopata uhalali kupitia MAHAKAMA.
CHADEMA sasa mahututi mbowe akikimbia. CCM kulamba dume.
UNA AKILI NYINGI SANA🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom