Probably matokeo yake hayatabiriki ila naweza kuongelea katika nukta hizi,
Kuondoka kwake huenda CHADEMA ikafanikiwa zaidi ya apo ilipo coz ukiongelea Chama unaongelea misingi na muundo(SHERIA, utaratibu, katiba, structure ya uongozi) hivyo vyote vitabaki huyo Mbowe akiondoka kwani hata CCM ilikuwa inaongozwa na Nyerere akaja Mwinyi mpk kufikia Samia Hassani.
Nukta ya pili akiondoka Chama Kinaweza kufa,Miaka takribani 10 amekiongoza Chama kama Mwenyekiti na amepitia mengi,anakijua Chama in-out hivyo waswahili wanaswma zimwi likujualo halili likakwisha.